Bei za mabasi

Arusha kuna Huge motors,wanapatikana Usa river,wanatengeneza body nzuri sana

Hughes Motors ni wauzaji wa magari, na si watengenezaji wa bodi za mabasi. Hayo mabasi ya Nissan Diesel yanayoonekana katika eneo la kampuni hiyo hapo Usa River yameigizwa kutoka Kenya yakiwa na bodi zake zilizotengenezwa na kampuni mbalimbali nchini humo kama Master Fabricators, Malva, Banbros na mengineyo.
 
Inshort yutong mpaka itembee barabarani kiasi cha 300million kinahitajika.

Na Yutong hiyo mpya kabla ya kuiweka barabarani inabidi uingie gharama ya kubadilisha ekseli (axle) ya nyuma kwa kuwa zinazokuja na mabasi hayo ni mbovu.
 

vipi kaka kama bado unahitaji mabasi tuwasiliane 0765032151
 
jukwaa la Baishara ni zuri jamii forum,majukwaa mengine yamevamiwa,Big up Bulldog
 
Mkuu wekeza kwenye Ardhi! Hebu tafakari hili!; > ile gari > ale dereva > ale konda > ile serkali > ale mpiga debe > ale polisi barabarani > ule mwenyewe! Hao wote mna ubia ktk ulaji lakini gari ikiharibika haiwahusu! Usishangae baada ya muda unakula sound tu! Sikutishi kama unaweza kuweka tuta nakutakia kila la Heri!
 

Yutong bei zake hizi hapa
Base Price:USD87,000.
AC: USD8,000.
TV:USD500
Luxury interior: USD3,000
Leather seats:USD4,000.
Fridge: USD500.
Usafiri: USD9,800

Pamoja
 
nunua nyumba seheme kama sinza, kijitonyama na nyingine kama hzo.... zikarabati hzo nyumba na kuipendezesha kisha pangisha au uza..... itakulipa kuliko hyo biashara ya mabasi ni risk na pasua kichwaa....utakonda bureee
 
Haya habari inaendelea,sijui kama muanzisha uzi yupo hai.

Sio kila mtu alime,wazo la kuanzisha Biashara ya magari sio baya.
Miaka ya 70 - 80 mtu alianza na gari moja tu,na hao ndio leo tunawaita Matajiri.
Hakuna biashara ambayo haina changamoto.
Ingekuwa hailipi basi viwanda vingefungwa na Yard zile za hapo Dar zisingeingia mikataba na Manufactures.
Naungana na mdau aliesema kwamba nunua hisa za Darts kama mdau,hapo itakulipa vizuri sana tu.
 
Nunua Costa upige dala dala. Ukipata zilizo kwenye hali nzuri hupati ugonjwa wa moyo. Pia risk ya ajali ni ndogo.
 
Mkuu huo mtaji mzuri sana aisee..

Njoo tuanzishe kampuni kubwa ya ulinzi kama G4S tuongeze pesa...

Kumbuka hapo tukuajiri elite working staff, basi tutapata malindo yasiyosumbua kulipa mwisho wa mwezi...

Kamata fursa twenzetu.
 

Mkuu kama hii mambo ndo bei gani ati? Halafu mkuu hapo bei si inategemea na chassis ni kampuni gani au marcopolo nao wana chassis zao?
 

Attachments

  • 1410427912548.jpg
    83.4 KB · Views: 870
  • 1410427963585.jpg
    75.2 KB · Views: 803
Safi nami nimepata elimu!

Kama sitokuwa nimeingilia uzi naomba pia nijuze wapi ntapata gari aina ya prado iliyotumika na inayotumia petrol, auto, ya 2000+, milango mitano, n.k
 
Nenda manzese,sinza nunua plots

I agree with you 1000 percent. Plot zitalipa. zitakuwa na hati utakopea kujenga hoteli watalala wanaokuja kufanya manunuzi kariakoo. si mnajua kariakoo inalisha most of EAfrican landlocked countries?
 
Mi biashara ya magari sitakagi kabisa kumshauri mtu, kaka nakuonea huruma. Halafu kuingia competititon na hao wachaga wa arusha na moshi ni kazi kubwa sana. Unaweza hata ufanyiwe hila vigari vyako 2 hivyo vipinduliwe viishilie na wewe mwenyewe kuishilia mbali kabisa.
 
INVEST KWENYE REAL ESTATE mf Nyumba au Viwanja vyenye hati baada ya mwaka ukiuza uko mbali na hina risk wala maintanance
UKIKOSEA TU, IMEKULA KWAKO
 
Mkuu kama hii mambo ndo bei gani ati? Halafu mkuu hapo bei si inategemea na chassis ni kampuni gani au marcopolo nao wana chassis zao?

Engine ni ya scania tu, mengine yanatoka marcopolo including chasis. Hyo inaweza kuwa mil 700 kila kitu
 

exactly hii kampuni ya masters iliyopo nairobi nchini kenya ni wazuri sana kwa kuunda body za magar coz nimechonga bas mbili huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…