kwa uzoefu wangu, basi zilizonzuri ni SCANIA, ingawa ni gharama sana.
scania moja si chini ya MIL 800 kaka, wakati mil 800 hizo unaweza pata Yotong 4,
kuhusu mabod ya kutengeneza check na BENBROS hawa jamaa wako vizuri sana kwenye mabod
Pia kama ulivyoshauriwa yotong hurudisha fedha haraka ingawa huchakaa mapema sana ukilinganisha na scania
hebu angalia magari ya SAIBABA, SCANDINAVIA ...hawa walikuwa wanatumia scania, na magali yao yalitumika muda mrefu
pia biashara ya mabasi bana usiwe na gari moja, utakufa pressa kaka, at least mawili au matatu, vinginevyo utanunua gari utakuwa umejinunulia ugonjwa bureeee!!
nakushari tafuta gari ndogo pia, MINBUS sio lazima zipige route kama daladala unaweza kutafuta kibali cha kwenda masafa marefu, au kuna magari aina ya fuso luxury sana utapata hata kwa mil 150-180. kisha unalipeleka dar tanga, au dar moro au dar iringa
Mkuu wekeza kwenye Ardhi! Hebu tafakari hili!; > ile gari > ale dereva > ale konda > ile serkali > ale mpiga debe > ale polisi barabarani > ule mwenyewe! Hao wote mna ubia ktk ulaji lakini gari ikiharibika haiwahusu! Usishangae baada ya muda unakula sound tu! Sikutishi kama unaweza kuweka tuta nakutakia kila la Heri!
Mkuu jenga nyumba kabla ya kustaafu, usitumie mafao ya kustaafu kujenga nyumba...Kweli JF ni kisima cha hekima
Ushauri mzuri sana huu
Kaka nenda kaongee na DAR EPRESS au MOHAMMED TRANS akuuzie basi zake zilizoanza kuchoka, Piga Rangi uanze mdogo mdogo. Route za DAR -MTWARA zinalipa sana
Nakushauri kama unauzoefu wa magari wa kutosha simaanishi gari ya kutembelea usifanye biashara hiyo pesa yako haitarudi ...
Nakupa ushauri wa bure kajenge nyumba za bei rahisi vyumba viwili au vitatu self container kisha upangishe utapata pesa nyingi sana na huku dhamani ikipanda.Pia wekeza kwenye viwanja ambavyo vinapanda dhamani nawe utakuwa bilionea ndani ya miaka 2 tu.Mkumuke Mungu katika shughuli zako.
kwa hiyo umeona dar-mtwara ndio kwa kupeleka mikweche? kwa taarifa yako mtwara zinaenda yutong za hatari akienda na hiyo migari yake mikuu kuu atabebea kuku na mbuzi tu bora unge mshauri apige ruti ya dar-mahenge,dar-handeni,dar kilosa,dar-mlalo,mtae,mlola na bumbuli,dar-mpwapwa,kondoa,bahi,au apige masafa ya dar-chunya,mbozi,kyela,dar-katavi,mpanda,nkasi,sumbawanga.
wewe nenda Dar coach utapatiwa kila kitu.Tutong zikichoka utajuta.
Hapo ndio atafilisika kabisa,
Nani kakwambia Kilimo kinalipa hapo jamaa yangu umemtupa kaburii kabisa.
hebu msaidie aje huku Dodoma kuna Mabasi ya kina Shukrani, Champion Shabibya au hata Mshikamano
cha kufanya kwa hizo 370m anunue mabasi 2 aweke Injini 2 mpya naye ajulikane mpingauonevu BUS SERVICE
Wazee ninakapesa fulani Mungu amenipatia lakini nataka kuwekeza kwenye biashara ya basi za abiria. Hivyo wapendwa wangu naomba ushauri
1. Bei za marcopolo ni TSHS ngapi? na bei ya YOUTONG ni kiasi gani?
2. Je ni basi gani ni imara ili nisiingie hasara likafa haraka?
3. Kama ni body za kuchonga bei zake zinaendaje na kampuni gani nzuri?
kwa wenye uzoefu je biashara ya mabasi inalipa?
mtaji wangu ni Milion 370. je inaweza nipatia mabasi mawili? maono yangu ni nilitaka kujaribu njia ya DAR -Arusha
Kwa sasa bei za Yutong hadi ikae barabarani ni bei gani?
180mil