Bei za mabasi

Bei za mabasi

Huyu mpingauonevu yuko wapi aje atupe mrejesho wa biashara yake, maana ni mwaka sasa tangh alete hii thread
 
Last edited by a moderator:
kwa uzoefu wangu, basi zilizonzuri ni SCANIA, ingawa ni gharama sana.

scania moja si chini ya MIL 800 kaka, wakati mil 800 hizo unaweza pata Yotong 4,

kuhusu mabod ya kutengeneza check na BENBROS hawa jamaa wako vizuri sana kwenye mabod

Pia kama ulivyoshauriwa yotong hurudisha fedha haraka ingawa huchakaa mapema sana ukilinganisha na scania

hebu angalia magari ya SAIBABA, SCANDINAVIA ...hawa walikuwa wanatumia scania, na magali yao yalitumika muda mrefu

pia biashara ya mabasi bana usiwe na gari moja, utakufa pressa kaka, at least mawili au matatu, vinginevyo utanunua gari utakuwa umejinunulia ugonjwa bureeee!!

nakushari tafuta gari ndogo pia, MINBUS sio lazima zipige route kama daladala unaweza kutafuta kibali cha kwenda masafa marefu, au kuna magari aina ya fuso luxury sana utapata hata kwa mil 150-180. kisha unalipeleka dar tanga, au dar moro au dar iringa

Benbros ni waagizaji na wauzaji wa mabasi ya Yutong Tanzania, na si kampuni ya kujenga bodi za mabasi. Mabasi ya Yutong na mengine ya Kichina huagizwa yakiwa complete (na bodi zake) kutoka China na wateja hupigiwa rangi za kampuni zao na kuandikiwa majina hukohuko China kama wakipenda.
 
Mkuu wekeza kwenye Ardhi! Hebu tafakari hili!; > ile gari > ale dereva > ale konda > ile serkali > ale mpiga debe > ale polisi barabarani > ule mwenyewe! Hao wote mna ubia ktk ulaji lakini gari ikiharibika haiwahusu! Usishangae baada ya muda unakula sound tu! Sikutishi kama unaweza kuweka tuta nakutakia kila la Heri!

Kweli JF ni kisima cha hekima
 
Kaka nenda kaongee na DAR EPRESS au MOHAMMED TRANS akuuzie basi zake zilizoanza kuchoka, Piga Rangi uanze mdogo mdogo. Route za DAR -MTWARA zinalipa sana
 
Ushauri mzuri sana huu

Nakushauri kama unauzoefu wa magari wa kutosha simaanishi gari ya kutembelea usifanye biashara hiyo pesa yako haitarudi ...

Nakupa ushauri wa bure kajenge nyumba za bei rahisi vyumba viwili au vitatu self container kisha upangishe utapata pesa nyingi sana na huku dhamani ikipanda.Pia wekeza kwenye viwanja ambavyo vinapanda dhamani nawe utakuwa bilionea ndani ya miaka 2 tu.Mkumuke Mungu katika shughuli zako.
 
Kaka nenda kaongee na DAR EPRESS au MOHAMMED TRANS akuuzie basi zake zilizoanza kuchoka, Piga Rangi uanze mdogo mdogo. Route za DAR -MTWARA zinalipa sana

kwa hiyo umeona dar-mtwara ndio kwa kupeleka mikweche? kwa taarifa yako mtwara zinaenda yutong za hatari akienda na hiyo migari yake mikuu kuu atabebea kuku na mbuzi tu bora unge mshauri apige ruti ya dar-mahenge,dar-handeni,dar kilosa,dar-mlalo,mtae,mlola na bumbuli,dar-mpwapwa,kondoa,bahi,au apige masafa ya dar-chunya,mbozi,kyela,dar-katavi,mpanda,nkasi,sumbawanga.
 
Nakushauri kama unauzoefu wa magari wa kutosha simaanishi gari ya kutembelea usifanye biashara hiyo pesa yako haitarudi ...

Nakupa ushauri wa bure kajenge nyumba za bei rahisi vyumba viwili au vitatu self container kisha upangishe utapata pesa nyingi sana na huku dhamani ikipanda.Pia wekeza kwenye viwanja ambavyo vinapanda dhamani nawe utakuwa bilionea ndani ya miaka 2 tu.Mkumuke Mungu katika shughuli zako.

labda umshauri kujenga nyumba na kuuza, lakini kujenga nyumba na kupangisha atazeeka.
 
kwa hiyo umeona dar-mtwara ndio kwa kupeleka mikweche? kwa taarifa yako mtwara zinaenda yutong za hatari akienda na hiyo migari yake mikuu kuu atabebea kuku na mbuzi tu bora unge mshauri apige ruti ya dar-mahenge,dar-handeni,dar kilosa,dar-mlalo,mtae,mlola na bumbuli,dar-mpwapwa,kondoa,bahi,au apige masafa ya dar-chunya,mbozi,kyela,dar-katavi,mpanda,nkasi,sumbawanga.

itoe dar mpwapwa maana ni youtongu na eicher tu hakuna mikweche huku
 
wewe nenda Dar coach utapatiwa kila kitu.Tutong zikichoka utajuta.
 
Hapo ndio atafilisika kabisa,
Nani kakwambia Kilimo kinalipa hapo jamaa yangu umemtupa kaburii kabisa.
hebu msaidie aje huku Dodoma kuna Mabasi ya kina Shukrani, Champion Shabibya au hata Mshikamano
cha kufanya kwa hizo 370m anunue mabasi 2 aweke Injini 2 mpya naye ajulikane mpingauonevu BUS SERVICE

Nasikia Zabibu zinalipa sana hapo Dodoma, kwa nini usimshauri afanye biashara hiyo???
 
Kanunueee scaniaa mendee used plus ushuru 120's M unufaike
 
180mil
 

Attachments

  • 1426317420121.jpg
    1426317420121.jpg
    70.8 KB · Views: 562
  • 1426317436874.jpg
    1426317436874.jpg
    66.6 KB · Views: 521
  • 1426317617334.jpg
    1426317617334.jpg
    90.4 KB · Views: 496
Wazee ninakapesa fulani Mungu amenipatia lakini nataka kuwekeza kwenye biashara ya basi za abiria. Hivyo wapendwa wangu naomba ushauri
1. Bei za marcopolo ni TSHS ngapi? na bei ya YOUTONG ni kiasi gani?
2. Je ni basi gani ni imara ili nisiingie hasara likafa haraka?
3. Kama ni body za kuchonga bei zake zinaendaje na kampuni gani nzuri?
kwa wenye uzoefu je biashara ya mabasi inalipa?
mtaji wangu ni Milion 370. je inaweza nipatia mabasi mawili? maono yangu ni nilitaka kujaribu njia ya DAR -Arusha


Mkuu naamini sijachelewa.

1. Biashara ya mabasi ni Biashara Kichaa Ukiwa na basi Moja lazima Ufiliske maana litakuwa la mawazo.

2. Ushahuri wangu nunua Yuoton sijuhi bei yalke lakini nilikuw anasikia jama wanatoa Mkopo, kwahiyo kw ahesabu z aharaka haraka nadhani unaweza ukanunua moja na jingine wakakupa mkopo( hii ni katika ile ile kuwa ni lazima uwe na basi kuanzia Moja ili hela uione.

3. naamini kama unaishi Arusha utakuw aunayajua magari(fuso) yanaitwa Capricon/Raqueb yale ni ya kuchonga na bei yake haifiki 100Mil, namini unaweza kutengeneza na ukapata magari MANNE(4) kama yake na ni imara japo madogo kwa rooti ya Dar arusha haiwezekani.

4. Root ya Dar Arusha sio laizma maana root nyingini za wilayani na mikoani zina hela nyingi kuliko hiyo unayotaka kwenda kwanza ni ndefu na abiria ni wa ushindani mkubwa.

5. Kuna magari yanaitwa TATA wacha hizi za UDA, kuna kubwa zake, mfano zipo zinaitwa "K" express zinatoka Arusha kwenda Turiani kupitia Tanga (Handeni) nilishaongea na konda na dereva na njia huko ni ya Vumbi na mbaya lakini wansema yale magari TATA katengeneza imara sana na ni chini ya 100Mil bei yake na najua TATA wankopesha pia. so unaweza kupata Matatu na ukayapeleka porini yakafanya vizuri.


Conclusion:
1. Nunua GARI zaidi ya moja.
2. Nunu zile Fuso za kutengeneza kwa watani zetu hapo ni cheap na Imara.
 
Back
Top Bottom