Mdau kuna watu wanakukatisha tamaa hapo juu ya hii biashara.
Kwanza nikwambie hii business inalipa sana, tena sana, ili mradi uwe na upate technic zake hasa kama utaweza kucheza na kitu nnachokiita (Udhaifu).
Twende kwenye topic, nijuavyo scania mpya kupitia kwa wakala wao mkuu pale nyerere road haizidi 700mil, yutong kupitia wakala wake benbros watakuchapa na 250mil, ukienda kwa manji -Dar coach kuchongewa body sina hakika sana ila si chini ya 100mil model mpya ya body na ukienda kenya kuna makampuni matatu ambayo ni famous sana kuna choda, LHS na nk.
Hivo basi kwa ushauri wangu mtaji wako ni mdogo kulingana na hitaji lako kwa gari la uhakika lenye uwezo wa kuishi kipindi kirefu.
Kwa hiyo nna ushauri huu hapa, nunua Yutong new model tena usitumie wakala wa hapa bongo ni PM nikupe simple, safe and preserve your money, hapo utapata mbili ambapo hata Sumatra watakupa kibali, kwani ukiwa na gari/bus moja hakuna kibali cha kwenda zaidi ya 320km.
Kwa habari ya kuibiwa na hao wakatisha tiketi kwa ufupi hakuna kitu kama hiyo ndg, ndo maana mdau mmoja kasema watu wasingenunua mabasi kama kuna hasara na wizi.
END.