Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wazee ninakapesa fulani Mungu amenipatia lakini nataka kuwekeza kwenye biashara ya basi za abiria. Hivyo wapendwa wangu naomba ushauri
1. Bei za marcopolo ni TSHS ngapi? na bei ya YOUTONG ni kiasi gani?
2. Je ni basi gani ni imara ili nisiingie hasara likafa haraka?
3. Kama ni body za kuchonga bei zake zinaendaje na kampuni gani nzuri?
kwa wenye uzoefu je biashara ya mabasi inalipa?
mtaji wangu ni Milion 370. je inaweza nipatia mabasi mawili? maono yangu ni nilitaka kujaribu njia ya DAR -Arusha
ndugu yangu nakushauri tu biashara ya mabasi ngumu unagawana na wauza tiketi
180mil
Bei 180mil zero km
Mkuu Nimevutiwa na iyo idea ya Eicher ebu fafanua kidogo nione pesa ivyorudi hapo [emoji39] [emoji39]Marcopolo 700Mil
Youtong 250 - 300 mil
Marcedes 800 Mil
Nakushauri nunua youtong, hela yako itarudi mapema.
Kwa hiyo budget sidhan kama utaweza hii biashara kwasababu utatakiwa kulipa insuarance ambayo si ya kitoto, kuna vipesa vitakutoka hapo vingivingi.
Kwa hiyo pesa nakushauri ununue Min buses za TATA au EICHER kama ma4 hivi yanauzwa 70Mil. Upige rote za mbezi - kkoo au mbezi - mwenge. Kwa mwaka unarudisha hela yako na mtaji utakuwa mkubwa na utakuwa umepata experience ya jinsi ya kufanya biashara ya mabus.
Hesabu ya bosi kwa bus la tata au eicher kwa siku ni 300,000Mkuu Nimevutiwa na iyo idea ya Eicher ebu fafanua kidogo nione pesa ivyorudi hapo [emoji39] [emoji39]