Bei za magari

Ilikuwa ni kampuni gani mkuu uliyowaelekeza?
 
Mi nimeagiza mwenyewe...
Nikabagain mwenyewe....
Nikalipia kila kitu mwenyewe...
Natarajia kupokea ndinga mwenyewe...
Maana ni yangu mwenyewe....

Shida ya Watanzania wengi ni uoga na kutishana.
Vipi ulipunguziwa dau zuri mkuu?
 
Vipi u
Hata gari za mkononi kibongo bongo gari bei chee ni mwanzo wa mwaka na mwisho wa mwaka. Maana purukushani za xmass, mwaka mpya na ada za shule huwafanya watu kuchizika na kuuza uza tu chuma kali bei chee! Gari zangu zote nimenunua nyakati hizo.

Hata gari za mkononi kibongo bongo gari bei chee ni mwanzo wa mwaka na mwisho wa mwaka. Maana purukushani za xmass, mwaka mpya na ada za shule huwafanya watu kuchizika na kuuza uza tu chuma kali bei chee! Gari zangu zote nimenunua nyakati hizo...
Vipi ulipata gari kali kwa bei nzuri maana wadau wanasema gari za mkononi hapa bongo risk ya kupigwa ni kubwa, gari mbovu inakufia mkononi
 
Usiagize gari hasa kama n mara ya kwanza n bora uwape watu wenye uzoefu wakuagizie wewe ukafate,ila ukisema uagize wewe kama wewe nadhani sio Mbaya ukijifunza kitu kwa utakachokutana nacho.
Hizo zama za kuwatumia watu kuagiza zimepitwa na wakati hata kama mtu hajui kutumia mitandao bado kampuni kama autocom, trust na mengine mengi tu yana ofisi zao Tanzania so ni mhitaji gari tu kwenda achague gari aitakayo anegotiate afanye malipo as kwa terms walizokubaliana then after 1 month gari hii hapa.
 
Hapo sasa umekanusha nini na kushauri nini? mimi najua unatoa solution ya namna gani aagize gari mwenyewe kumbe upo mule mule aende akaagiziwe.

mshauri aagize mwenyewe yeye kama yeye,maana ushasema zama za kuwatumia watu zimepitwa na wakati.
 
Hapo sasa umekanusha nini na kushauri nini? mimi najua unatoa solution ya namna gani aagize gari mwenyewe kumbe upo mule mule aende akaagiziwe.

mshauri aagize mwenyewe yeye kama yeye,maana ushasema zama za kuwatumia watu zimepitwa na wakati.
Kumbuka nimetoa namna mbili ya kwanza ni kama yupo conversant na mitandao anaagiza tu mwenyewe ya pili kama hayupo conversant na mitandao ndo sasa anaenda tawi la kampuni husika ya japani inayoheshimika lilopo Tanzania na nimetaja kampuni kwa mfano trust ni kampuni ya wajapani na hawana longolongo hata matawi yao yanaeleweka watamsaidia. Ninachosema kimepitwa na wakati ni eti kwa mfano uende kwa madalali wa kibongo waliojaa magomeni, mwenge, dodoma ambao hawana physical stock yoyote ya gari japani (ila wana stock za picha za magari kama zote kwenye vilaptop vyao) then wao ndo waanze process za kumuagizia mtu hii hapana maana kwanza kampuni nyingi hizi hazina uwazi, pili lazima wapige sana vya juu mwishowe mnunuzi ataishia kununua gari bei juu, mileage imeenda mnooo ingawa picha ataonyeshwa yenye mileage ndogo, ataonyeshwa gari ya grade ya chini ilihali yeye ataambiwa ni grade ya kwanza au pili. Vile vile wakiona mteja kolo hata kodi na tozo za bandarini watampa amount kubwa na watataka wakalipie wenyewe ila asijue nini kinaendelea.
 
Haiwezekani kutapeliwa chamsingi angalia tu kampuni unayotaka kuagiza owe list ya kampuni za wauzaji wa magari used kwenye website ya chama Chao, hata hao mnaoona waaminifu wanaogopa hiki chama ukilalamika TU umetapeliwa utakuwa refunded na wahusika wanapigwa fine yakufa mtu sema waagizaji wengi hawalijui hili.
Nimekuwa nikiagiza kupitia kampuni ndogo yaani unabembelezwa mpaka upokee gari lako na ukishalipokea unasumbuliwa uwatumie picha ya testimonies ili waweke kwenye website yao
 
Vipi ulipata gari kali kwa bei nzuri maana wadau wanasema gari za mkononi hapa bongo risk ya kupigwa ni kubwa, gari mbovu inakufia mkononi
Kumbuka wabongo wengi huuza gari kwa kuwa limemshasumbua yaani shipa ni mara chache ununue gari kwa mbongo halafu ipo katika hali nzuri. Kingine kumbuka kwa mfano unanunua gari kwa mtu ambaye ana kipato cha kuungaunga chances ni kubwa kuwa hilo gari lake litakuwa halikuwahi kuwa na service history nzuri, na kuna gari ukisikia la mtu wa jamii fulani/hadhi fulani na anaishi mahali fulani unajua at least utapata kitu chenye uafadhali. Ila ukibahatika sometime kuna gari nzuri waweza pata halafu bei chee.
 

Napenda kuzijua hizo kampuni nyingine

Nazofahamu ni
1.SBT
2.Autocom
3.Beforward
4.Enhance
5.japannesevehicles
6.Real Motors
7.hebu ongeza list watu wajue machimbo
 
Fafanua 3.5 na hiyo Grade R Mkuu. Huenda tunapagawa na Bei kumbe tunabeba skrepa
 
Kwa uzoefu wangu gari ni best ukaagiza mwenyewe mwenye show room anaagiza kama wewe tu ila yeye anaagiza kibiashara zaidi anaweza akaagiza ATA gari Tano zikatoka siku moja kwaiyo ukienda kwake kununua lazima akupigie Cha juu sababu yeye kashaitoa bandarini kaweka ofisini kwake WAJANJA huwaga Wana import WENYEWE gari zao kutoka Japan
 
Mkuu kwa ushauri mzuri agiza Gari mwenyew tu tena ni rahisi haina complications Sana Tumia hata siku 2 kusearch mtandaoni mfano mm niliagiza Toyota ist Japan nikawa napitia Karibu magari 40 then nkachagua Moja zuri ambalo limo ndani ya uwezo wangu nikamcontact seller moja kwa Moja akanitumia bei kwa profoma nikaomba na discount mwenyew nikapewa nikalipia kwa kutumia NMB bank (nilienda physically bank kabsa) then Gari ikatumwa gari ikikaribia TZ hua wanatuma documents za Gari kwa ajili ya Ku clear bandarini then utamkabidhi agent unayemuamini atakutolea Gari Yako so haina haja yakutumia third party kilak2 kiko wazi Kama Una swali ulizia Hapa Hapa Ili wengne nao wapate elimu wasiwe waoga, hizi showroom wamezidisha janja janja Sana na kutuuzia Gari zilizoshushwa km
 
Asante mkuu umeeleza vizuri sana nimeelewa ngoja nifanye mchakato
 
Hizi gari nzuri za bei chee utazipata endapo utakutana moja kwa moja na mmiliki anayeiuza tofauti na hapo ikipitia kwa madalali lazima waipandilie bei issue inakuja ni connection kati yako na mmiliki utajuaje kama kuna gari inauzwa bila dalali ni Bahati sana ila wapo wamiliki wanaouza magari mazuri kwa bei cheap sana unakuta kuna mtu yeye anabadilisha gari kila mwaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…