Bei za Smartphone mbona hazishuki?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Nyanja: Biashara


Taswira zote kwa hisani ya Google​

Kwenye kikao cha Bunge la bajeti kilichokwisha 2021-2022 Mhe. Waziri wa Fedha aliwasilisha kwamba tozo kwenye manunuzi ya simujanja na vishkwambi zitapunguzwa ili wananchi wengi wamudu kuzinunua ili matumizi kwenye data yawe na watu wengi ambao watalipa tozo za data kwa wingi na serikali na makampuni kujipatia mapato zaidi kwa ajili ya maendeleo yao licha ya wananchi pia kufaidi matunda ya mawasiliano bora.

Nimefanya survey kwenye maduka ya gadgets hizi Kariakoo na Posta, cha ajabu ni kwamba bei hazijabadilika katu na wengi wanaendelea kumiliki vitochi ambavyo haviwezi kuziingizia serikali na makampuni ya simu mapato mengi tarajali kwa ajili ya maendeleo. Tatizo ni muaandaji wa bajeti ile au mtekelezaji wa bajeti ile? au Wananchi wasiokuwa na pesa? Au wote watatu kwa pamoja?

Ufumbuzi:
Serikali ichukuwe hatua za makusudi kabisa ama kuruzuku au ku-guarantee makampuni ya simu au hata TTCL-Mobile pekee na Airtel ambapo serikali inamiliki hisa ili ziagize vifaa hivi kwa wingi na kuwa mwanzo wa bei kushuka sokoni (Multiplier effect).
 
Kama hazishuki mkuu zifate huko huko juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…