Bei za vitu kushuka Kenya, sisi tunakwama wapi?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kufuatia maandamano ya kizalendo Kenya, serikali ya huko, imeamua kushusha bei za vyakula.



Upinzani unataka bei ya unga kwa kilo isizidi 2,000/- za kitanzania, vinginevyo wanarudi Tahrir.

Bei ya Unga itashuka kuanzia wiki ijayo, Rais Ruto aahidi


Hakuna mahali popote Kenya (au kwingine) wanakodai kuwa hizi ni harakati za wajaluo au kuwa hata ni za kikabila, isipokuwa Tanzania. Maana kamili ya kuwa mtanzania ni mjuaji mno!

"Hivi pilipili usisozila zinakuwasha nini?"

Wakenya wana matatizo Yao wanayoyatambua. Kwamba ni yao na kuwa hawana mjomba wala shangazi wa kuwatatulia.

Wanajua mfumbuzi wa matatizo yao ni wao wenyewe. Hawatafuti visingizio, mchawi wala kujaribu kuyakimbia. Wanajua matatizo hukabiliwa, tena kwa vitendo si kwa maneno.

"Maneno matupu hayavunji mfupa."

Inafahamika kuwa hata huko walamba asali, wahuni na hata vijana wa hovyo wapo. Kwamba yaliyoko kwetu na kwao yapo. Hata hivyo ujasiri wa viongozi wao wenye misimamo isiyotetereka ni jambo la kupigiwa mfano sana.

Kushuka kwa bei za bidhaa muhimu Kenya ni kwa manufaa ya wakenya wote.

"Liko kama mtego wa panya wenye kunasa waliomo na wasiokuwamo."

Tunataka haki? Hatutaki tozo? Tukutane Tahrir.

Huu ndiyo ulio ukweli mchungu. Mengine yote ni manjonjo tu.
 
Jibu hoja usi attack personality. Ubadhirifu ni jambo moja na inflation ni lingine. Tuna kazi kubwa sana kama taifa kuutokomeza ujinga

Suala la utawala bora lina maana yoyote kwako? Au ni mpaka nikuwekee picha halisi za mabulungutu ya noti na wezi wetu?



Wapi nilipo attack personality? Kulikoni kuniwekea maneno mdomoni ndugu?

Tofautisha swali na kauli (statement).

Angalizo: Vinginevyo inaweza kuwa muhimu kufahamu kiwango chako cha elimu Ili kujua scope ya mjadala.

"Kwa kweli tuna kazi kubwa sana ya kuutokomeza ujinga kama wako, Tanzania."
 
Sasa serikali ipo kwa manufaa gani kiongozi?

Kwa kukusaidia tu government policy zina determine market force. Hiyo ni commerce form two

Ninakazia: tatizo letu ni kuwa mtanzania ni mjuaji mno!
 
Mkasome ata cheti cha upishi, mko empty sana vichwani
Hujui na unajiona unajua hutaki kuelimishwa ...Hayati Mwl. Nyerere alishafafanua aina hii ya watu akielezea tofauti ya wajinga na wapumbafu(fools)!!!. Wewe ni wakuonewa huruma tuu
 
Hujui na unajiona unajua hutaki kuelimishwa ...Hayati Mwl. Nyerere alishafafanua aina hii ya watu!!!. Wewe ni wakuonewa huruma tuu
Mimi ndiyo elimu yenyewe, kama utaki andamana kama baba yako Odinga
 
Ni aibu sana kwa taifa na vijana kama hawa. Ana mchango gani huyu kwenye taifa hili.
Mkuu haupo sahihi na MIXOLOGIST amekujibu vizuri tu. Wewe unapinga for the sake of kupinga na una cherry pick data.

Yapo mataifa ambayo yamehandle huu mfumuko vizuri ila Kenya si mmoja wapo na Serikali hapa Tz imejitahidi sana.

Wakati wao hata hela ya kulipa mishahara hawana sisi tunatangaza ajira mpya. Kuna maelfu ya bidhaa ni Bei rahisi zaidi Tanzania kuliko Kenya, Petroli tu haijawahi kushuka Equivalent ya 3000 huku Kwetu kipindi cha karibuni.
 
Waeleze hao vilaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…