Hapa hatukomai tunayosimamia wala kiimani bali tunajadiliana kwa hoja kutambua changamoto zinazotukabili. Tofautisha mijadala ya kidini ambako tunayosimamia yaani imani ndiyo yanayojadiliwa.
Inafauhamika kuwa tofautiana kwa hoja kwenye harakati zozote za ukombozi ni jambo la afya tu ndugu.
"Kwamba iifano ninayotoa kuwa haiendani na unachokizungunzia?"
Ninadhani zaidi sana unachokizungunzia ni kuwa watanzania ni waoga. Hilo ninalipinga kwa hoja. Si sahihi kudhani JKNIA LIssu #1 au Kiluvha showdown zilikuwa nyepesi kama kihivyo.
View attachment 2590428
Hao walikuwa mamwela wavunja miguu ya watu wenyewe tena kwenye ubora wao.
Kipindi hicho Sirro na Mambosasa walitaka asiende mtu JKNIA vinginevyo angevunjwa miguu. Lissu Kiluvya njiani kwenda pwani ilikuwa hivyo hivyo.
Ninadhani hukuwepo kwenye matukio mawili haya kiasi kwamba kutaka kuyadogosha hivi ni mambo kushangaza sana. Hii ndiyo Ile waswahili wanasema mzigo wa mwenzio kwako ni kama kanda la sufi. Sidhani kama Lissu anakubakiliana na petty statements kama hizi za kuwa hizo zilikuwa sherehe.
Mengine uliyoandika sasa kwamba umeikana hadithi ya kuhalalisha kulamba asali, beberu anasema yanakuwa trivial. Yaani kwa kiswahili yanakuwa mwenye macho haambiwi tazama. Kimahesabu inakuwa ni sawa na namba + 0.
Hukuandika lolote kuhusu kuangaliana usoni kwa maana yake kamili. Mfano ziko moral obligations za waume wa ma COVID 19 kuendelea kuwa viongozi wetu?
Hukuandika lolote kuhusu nyomi ya angalau wanachadema 2,000 kwenye kuweka mazingira ya kutokamatwa Mbowe, wala hata kutambua tu kwamba BAVICHA ni Chadema pia.
Kwa sababu ya issues za muda niombe tuwe tayari kusoma rejea za posts na nyuzi. Kuandika jambo lile lile mara kibao hakuwezi kuwa na tija.
Kwa hapa ni kurejee kwenye post niliyomjibu bwana
Allen Kilewella nikimwomba (bila mafanikio) tuwe na msingi mmoja wa majadiliano badala ya hii ya kuruka ruka huku na kule.
Kwangu post hiyo ni namba 124. Kwenye post hiyo nilikuwa nimeainisha hoja zake sita ambazo nilizijibu kwa mapana na marefu yake.
(a) Kwamba watanzania ni waoga.
(b) Kushindwa kutambua umuhimu wa Raila kwenye mapambano haya.
(c) Maandamano huratibiwa.
(d) Kumhusu Liz Truss.
(e) Siyo Kenya yote inayoandamana.
Ninatambua huyo bwana kama ilivyokuwa kina
joni,
Paskali na wenzao walichagua kutokuwa wameiona.