Bei za vyakula yashuka nchini

Bei za vyakula yashuka nchini

Kwa msiojua kipindi hiki ni cha mavuno, msishangilie sana. Huku niliko mchele kilo moja ni 1700 mpaka 1600.

Ikifika mwezi wa 8 hadi wa 12 mje mlete mrejesho kama kilo ya mchele haitakuwa ni sh.4500/=[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Avunje ndoa gani huyo analala sebuleni kwa dada yake, atajua wapi bezi za vyakula.
MI siulizagi bei napimiwa mzigo nnaotaka namuuliza jumla unanidai sh ngapi, imeisha hiyo. Mambo ya kukalkuleti mpaka bei ya nusu kibaba cha mafuta nikuikaribisha roho ya umaskini.
Tumia ikiisha mnashinda njaa, kufunga sunna sio mpaka uuone mwezi
 
Ndugu zangu leo nimestaajabu pale wife aliponiambia, mchele sasa hivi kg moja inaanzia 2400 kwa kilo hadi 3000.

Tofauti na hapo awali bei ilikuwa inaanzia 2800 hadi 3500 kwa kilo.

Mafuta ya kupikia nayo yameshuka kutoka 4500 kwa lita hadi 3800.

Maharage na mahindi nayo yamashuka kwa kiwango kikubwa.

Vipi ndugu zangu huko mlipo bei zipoje?
Mtaani kwetu mchele mpya unaanzia 2000 na wa zamani ndio 2800 na kuendelea. Mimi napenda mchele wa zamani ambao ni mgumu mpya home mara nyingi unapikwa na kuwa boko
 
Ndugu zangu leo nimestaajabu pale wife aliponiambia, mchele sasa hivi kg moja inaanzia 2400 kwa kilo hadi 3000.

Tofauti na hapo awali bei ilikuwa inaanzia 2800 hadi 3500 kwa kilo.

Mafuta ya kupikia nayo yameshuka kutoka 4500 kwa lita hadi 3800.

Maharage na mahindi nayo yamashuka kwa kiwango kikubwa.

Vipi ndugu zangu huko mlipo bei zipoje?
Muulize vizuri huyo shemeji. Isije ikawa Kuna mtu anachangia Sasa ili usistuke anakuambia Bei zimeshuka.
 
Ukiamua tafuta vyakula vimeshuka bei
 
Ukiamua tafuta vyakula vimeshuka bei

Wakati kama huu unanunua mpunga gunia kadhaa, maharagwe, mbaazi, mahindi unanunua ile mifuko spesho isiopitisha hewa unatunza chakula walau cha kukufikisha mwakani, unabaki unapambana na vitu vidogovidogo, wengine wanalia wewe unawachek tu
 
Miezi ambayo bei inakuwa chini ni michache tu ukilinganisha na miezi ya kufunga mikanda.

Kama upo vizuri nunua mahitaji ya familia yako sasa halafu kausha by October tu hapo wakulima washauza hadi mbegu nao wanahemea.
 
Wakati kama huu unanunua mpunga gunia kadhaa, maharagwe, mbaazi, mahindi unanunua ile mifuko spesho isiopitisha hewa unatunza chakula walau cha kukufikisha mwakani, unabaki unapambana na vitu vidogovidogo, wengine wanalia wewe unawachek tu
Kama mfanyabiashara ila kwa sisi ambao kwa mwaka hatumalizi gunia zima la mchele hapana
 
Ndugu zangu leo nimestaajabu pale wife aliponiambia, mchele sasa hivi kg moja inaanzia 2400 kwa kilo hadi 3000.

Tofauti na hapo awali bei ilikuwa inaanzia 2800 hadi 3500 kwa kilo.

Mafuta ya kupikia nayo yameshuka kutoka 4500 kwa lita hadi 3800.

Maharage na mahindi nayo yamashuka kwa kiwango kikubwa.

Vipi ndugu zangu huko mlipo bei zipoje?
Hongera zake Samia
 
Back
Top Bottom