Je, kuna mawazo yoyote kuhusu jinsi Tanzania inavyoweza kujipanga ili mwaka 2012 historia isijirudie?
Tanzania tunao watu wenye vipaji vingi sana(hasa vijijini),,,ni kiasi cha TOC kwenda vijijini na kukusanya watu wenye vipaji kisha kuwafanyia maandalizi kwa ajili ya 2012 Olympic games,,,,mfano Wahadzabe ni wataalamu sana wa kurusha mishale(wanatisha),,,,Wasukuma ni wazuri sana kwa baiskeli,,,,Wamasai wanatisaha katika urushaji wa mikuki,,,,,,kuna Wakisi na Wamanda wa Ludewa hawa jamaa ni mwisho kwa kuogelea,,,,,,,,kua Wanyaturu,Wambulu,Wabarbaig na Wairak wao ni wazuri sana katika Riadha.....Kimsingi vipaji vipo vngi sana huko vijijini ni kiasi cha TOC kwenda vijijini na kufanya scouting ya hawa watu na kuwafundisha njia za kisasa za kurusha mishale,kutupa mikuki,kuogelea,kuendesha baiskeli,Riadha pamoja na michezo mingi tu ambayo Tanzania kuna watu wana vipaji nayo ila wamekosa nafasi ya kuvionesha