FAJES
JF-Expert Member
- Oct 29, 2017
- 720
- 644
TANGAZO LA KAZI TAREHE 23, DISEMBA 2020.
BEITO IINTERNATIONAL COMPANY LTD, tunajihusisha na shughuli za usafi na urembo. Ofisi zetu zipo Dar es Salaam, Wilaya ya Kinondoni, Mwenge, ITV.
- Tunatangaza nadfasi za kazi kwa vijana wa kike na kiume wenye vipaji na ujuzi wa kutoa huduma zifuatazo Jijini Dar es Salaam.
- Kipaji cha kusuka mitindo mbalimbali
- Kipaji cha kunyoa mitindo aina mbalimbali
- Kutengeneza na kupaka rangi kucha
- Kufanya MAKE-UP
- Huduma zetu tunawafuata wateja mahali walipo hasa hasa majumbani kwao.
- Muda mfupi ujao, wateja wetu watakuwa na uwezo wa kuomba huduma kwa njia za kidijitali (kupitia website na mobile- App) hivyo kwa baadae siyo sasa) watoa huduma wetu watatakiwa kuwa na Smartphone ili kupata acess ya kuwasiliana na Ofisi yetu na wateja wetu.
- Uaminifu wako ni sifa kubwa zaidi tunayohitaji
- Uwe na haiba na tabia njema isiyo na mashaka
- Mchapakazi na mwenye kujituma
- Msafi na Mtanashati
- Mkweli, mcheshi na mkarimu
- Uwe unaishi sehemu yoyote Dar es Salaam.
- Ujue kusoma na kuandika
- Ujue kutumia Smartphone
- Mwenye uzoefu wa kuanzia angalau miezi 6 atapewa kipaumbele
- Fika mwenyewe katika Ofisi zetu zilizopo Mwenge ITV, Bagamoyo road kwa ajili ya usaili mfupi na kuanza kazi maramoja.
- Fika kati ya Jumatatu hadi Ijumaa; muda kuanzia saa 3 asbh - 10 Jioni.
Fika na nyaraka zifuatazo.
1.Barua ya maombi ya kazi, ikiainisha aina ya kazi unayohitaji kufanya, unaruhusiwa kuomba kufanya kazi zaidi ya moja kulingana na uwezo wako
Maombi yatumwe kwa;
Mkurugenzi Mtendaji,
BEITO International Company Ltd
S.L.P 391,
Dar es Salaam.
2. Barua ya Utambulisho kutoka Ofisi ya Mtaa
3. Uthibitisho kuwa haujawahi kuhusika na makosa ya jinai kutoka kituo cha Polisi unapoishi (Ni muhimu lakini siyo lazima).
4. Nakala ya kitambulisho cha Taifa (NIDA) au kitambulisho kingine kinachotambulika.
5. Barua ya mdhamini na mawasilino yake ( anaweza kuwa ndugu, mwenza au mzazi).
6. Cheti kama unacho (siyo lazima) chochote kinachoendana na aina ya kazi unayoomba.
MALIPO
- Watoa huduma watakaokuwa wamejiajiri (Freelancers) watapata malipo ya aslimia 70 (70%) ya malipo ya kazi husika.
NOTE: Tangazo hili limetolewa kuanzia leo tarehe 23 Disemba, 2020. Mwisho wake itategemea na kiasi cha watoa huduma watakaopatikana kwa wakati huo.