Beki bora wa Tanzania miaka ya nyuma ni nani?

Lenny, Mored,Wastara na Beya Simba hawakuwa mabeki mazee..
 
Beki kisiki aliye dumu sana ktk timu ya taifa alikuwa Mohammed Chuma. Huyu alikuwa chinga kama kumbukumbu zangu ziko sahihi alikuwa akichezea timu ya bandari Mtwara.

Kweli kabisa. Mohamed Chuma alicheza kama beki we timu ya Taifa kwa miaka.mingi sana
Wengi tunamkumbuka Ile miaka ya 60 na 70.
 
Constantine Kimanda,Banza Tshikala,Said Mwamba Kizota,Paul John Masanja,Bakari Malima Jembe Ulaya,John Mwansansu,Keneth Pius Mkapa.
 
Jamani mme msahau GORDWIN ASWILE MRIMBA.. jamaa nguvu kazi.
 
Keneth Mkapa na George Masatu
 
Combination bora kabisa ilikuwa ya Constantino Kimanda na Method Mogella "Fundi" wakati amerudi kucheza nyuma kutoka kiungo

Mkapa Kenny, Banna Yusup ismail, mwakalebela, Minziro hawakuwa wabaya pia
 
yaani kwa wachezaji hawa unakuwa na hamu ya kwenda kuangalia mpira lakini sasa hakuna mpira kuna uhuni WATU WANAKWENDA KUMWANGALIA ali yanga.
 
Jobe ayoub kwasakwasa (sijui nimevamia thread!?)
 
Ramadhan Wasso, Quresh Ufunguo,Aboubakar Kombo, Yusuph Lazaro, Willy "Mtenda wema"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…