Beki Juma Nyosso ameachiwa kwa dhamana na klabu ya kagera imesema haitomuadhibu beki huyo

junky

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2017
Posts
413
Reaction score
978
-Beki wa Klabu ya Kagera Sugar, Juma Nyoso aliyekuwa ameshikiliwa na jeshi la polisi mkoani kagera kwa kosa la kupiga na kujeruhi ameachiwa kwa dhamana leo asubuhi.

-Jeshi la polisi mkoa wa Kagera wamesema wanaendelea kupeleleza zaidi huku kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Kagera Isack Msangi akifichua kuwa endapo ikibainika shabiki aliyepigwa na Nyoso alifanya kosa la jinai la kutukana hadharani atafikishwa mahakamani naye kujibu shitaka hilo.

-Moja kwa moja Nyoso amejiunga na timu yake ya Kagera kwa maandalizi ya mchezo wa jumamosi hii january 27 dhidi ya Lipuli Fc Mchezo utakaochezwa katika dimba la Kaitaba Bukoba. Pia klabu ya Kagera sugar imesema haitomwadhibu mchezaji huyo kwa kile alichokifanya.

-Pia Klabu ya Kagera imeandika barua kwenda kwa wamiliki wa uwanja wa Kaitaba, Chama cha soka mkoa wa Kagera na Bodi ya Ligi kuwasihi wasiwe wanaruhusu mashabiki kuingia kwenye uwanja baada ya mchezo kuisha.

NB: pongezi kwa uongozi wa Kagera Sugar

Hapa kazi tu[emoji23] [emoji23]

Mgonjwa anaendelea vizuri
 
Mashabiki pia wajue kuna limit ya kuzomea haiwezekani mchezaji atukanwe hadi matusi ya nguoni, ya kifamilia kabisa afu mseme eti ndo ushabiki!! Hilo hamna kabisa na kwa mchezaji kama Nyoso kufikia kufanya kitendo cha hivo haukuwa ushabiki wa kumzomea tu!! Tusiwahukumu tu wachezaji bila kujua hata wao wametendewaje???
 
Natumaini hata TFF hawatampa adhabu kubwa huyu jamaa.

..........Mashabiki wanakela sana.
 
Hiyo Ni kweli mkuu, mashabiki wengine uwa wanawashwawashwa , hila nimeipenda kauli ya polisi ya kutaka kumfungulia mashtaka ya kutukana na kudhalilisha huyo shabiki , tena anatakiwa afungiwe kuingia uwanjani
 
Hii ipo bongo tu,ulaya shabiki akiingia uwanjani hata akimzogoa mchezaji haruhusiwi kumpiga, shabiki atapewa adhabu yake kwa kuingia uwanjani,mchezaji atapewa adhabu ikibainika alimpiga shabiki. Hapa nasubiria TFF watasemaje
 
Mkuu mpira ulikuwa umeisha ndio maana polisi wakaingilia
 
Hii ipo bongo tu,ulaya shabiki akiingia uwanjani hata akimzogoa mchezaji haruhusiwi kumpiga, shabiki atapewa adhabu yake kwa kuingia uwanjani,mchezaji atapewa adhabu ikibainika alimpiga shabiki. Hapa nasubiria TFF watasemaje
Umesaha juzi tu hapa Patrice Evra kampiga shabiki
 
Mzee Huku ni Ulaya?
 
Reaction ya nyosso ni sahihi kabisA Maana huyu alikuwa anamchokoza juma ili iweje kipigo kwake kilistahili kabisa
 
Hivi nyoso si ndo alipiga vidole watu matakoni
 
eric cantona pia alimpa mtu kick kama jet li vile

Umesaha juzi tu hapa Patrice Evra kampiga shabiki
Hawa wote waliwapiga mashabiki wakiwa sehemu zao(jukwaani)
Ila huyu kwa nyoso ni mshabiki katoka huko alikotoka kaenda kumzonga mchezaji, kamtusi na kumpulizia vuvuzela juu, huu si ushabiki ni upopoma, mie kibongo bongo naipenda simba lakin huyu shabiki mwenzetu alileta mambo ya kishamba, watu watamlaumu nyoso lakin tujiulize tu kama lile vuvuzela lingekuwa ni kisu je, tungekuwa tunaongea mengine.. Kilichomponza nyoso ni ile background yake ila angefanya mtu kama kaseja ambae hana mambo ya kipuuzi huko nyuma saa hizi nahisi lingekuwa limeisha na tanzania nzima ingekuwa inamlaumu huyu mshabiki mbuzi na ushabiki wake wa kiboya boya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…