Tetesi: Beki kisiki Kasaini tena Yanga

Tetesi: Beki kisiki Kasaini tena Yanga

Smart codetz

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2023
Posts
218
Reaction score
875
Mlinzi wa kati mwenye uwezo wa kukaba hadi upepo Dickson Job amesinya mkataba wa miaka miwili kuendelea kutwanga/kucheza Yanga,ni suala la muda kwa Yanga kutangaza taarifa zake, bwana mdogo bado ni wanjano na kijani hivyo bado atakua pale kwenye ukuta wa Yanga!!.

Ikimbukwe job alikuwa na kwenye Mazungumzo ya muda mrefu ya kusaini kandarasi mpya na waajili wake baada ya mkataba wa mwanzo kuwa ukingoni.
0390960C-9EB0-41D7-8121-6DF678C01D70.jpeg
 
Unajua maana ya kisiki muulize Mechi ya al hilal hataki kuwasikia huyo ndugu yake Job ndugai
 
Unajua maana ya kisiki muulize Mechi ya al hilal hataki kuwasikia huyo ndugu yake Job ndugai
Alicheza vizuri sana Ile game sema wale jamaa walijua Kutumia kosa Moja pekee kufanya matokeo yawe yalivyokuwa ila kwa Sasa ni beki mzuri sana na daraja sahihi kwa Yanga
 
Huyo beki mfupi hachezi header balls sisi wa nini 😀 😀 😀
 
Mlinzi wa kati mwenye uwezo wa kukaba hadi upepo Dickson Job amesinya mkataba wa miaka miwili kuendelea kutwanga/kucheza Yanga,ni suala la muda kwa Yanga kutangaza taarifa zake, bwana mdogo bado ni wanjano na kijani hivyo bado atakua pale kwenye ukuta wa Yanga!!.

Ikimbukwe job alikuwa na kwenye Mazungumzo ya muda mrefu ya kusaini kandarasi mpya na waajili wake baada ya mkataba wa mwanzo kuwa ukingoni.
View attachment 2588365
Amesaini mpunga wa maana, hatutaki ya fei hapa
 
Huyo beki mfupi hachezi header balls sisi wa nini 😀 😀 😀
Halafu sijui huwa mashabiki huwa hawaoni udhaifu huu. Hata mchezaji awe mzuri vipi kukaba kwa miguu ila akiwa mfupi ni kazi na bure kucheza beki ya katikati.
 
Halafu sijui huwa mashabiki huwa hawaoni udhaifu huu. Hata mchezaji awe mzuri vipi kukaba kwa miguu ila akiwa mfupi ni kazi na bure kucheza beki ya katikati.
Lisandro Martinez wa Man U ni Mrefu???
Je Maguire Ni Mfupi??
From there kati ya Lisandro na Maguire yupi anafanya Makosa sana Pale Man U??
Bro Mpira siku hizi ni Akili sio hizo Natural Factors na ndio maana siku hizi Mpira unaendeshwa kwa Academy nyingi sio Talents..Talents zipo ila zimekua kidogo.
 
Wechezaji wazawa wenye akili kama huyu ni wachache sana, mkataba unakaribia kufikia ukingoni Menejimenti ya mchezaji wamekaa mezani na Timu wamekubaliana na kuongeza mkataba na si kama yule Zuwena kukimbia kambi na kuanza kupiga kelele kama waimba taarab!

Back
Top Bottom