Belarus inaelekea kuwa kama Venezuela na baada ya hapo ni Tanzania?

Hatari kutokea Ukraine kwenda Belarus sio kutoka maeneo yenye usalama hafifu bali ni kutokea moja kwa moja kwa serikali iliyo madarakani sababu ni serikali inayofuata sera za magharibi na kwa kiasi kikubwa iliwekwa na mataifa ya magharibi, hivyo majasusi wa maadui wa Belarus wapo huru kuamua kutumia nchi ya Ukraine kuhujumu serikali ya Bwana Alexander Lukashenko.
Lukashenko anaziona serikali za Lithuania, Poland na Ukraine kama zilizo tayari kusaidiana na mataifa ya magharibi kumng'oa madarakani ndio maana anataka kufunga mipaka ya nchi yake dhidi ya nchi hizo
Ni kama Marekani ilivyotaka kutumia Columbia kupenyeza mamluki wake kwenda kumng'oa Nicolaus Maduro wa Venezuela
 
Asante kwa masahihisho mkuu ila China inahitaji ccm iendelee kutawala kuliko mshindani wa ccm kwa sasa ambaye amekiri hadharani kuwa ataendesha nchi kwa mfumo wa kimangaribi. Hata rais tuliye nae kwa sasa anaona heri wakomunisti kuliko mabeberu
 
Duh hatimae mwamba mwingine unatikiswa kwa nguvu na wenye nguvu. Poleni wabelorussian
 
Sasa Tanzania hapo inaingiaje mkuu? Au ulitaka kumuomgelea huyu kibaraka wa mabeberu mheshimiwa sana lissu
Maajabu ya dunia kibaraka wa mabeberu, anapo myima raha mzalendo wa taifa!!! Kwani haamini anacho kiona, ila kuna funzo awamu hii atakuwa amelipata!!
 
Rais Magufuli ni Kiongozi mzuri sana kwa ustawi wa Tanzania ya kweli, kama atatawala Miaka 10 Nchi yetu itakuwa na nguvu sana kiuchumi, Chini ya utawala wake Wazungu wametikiswa sana, Hawana ushawishi kwa Tanzania.
Ameonyesha kwa vitendo kuwa tunaweza kusimama kama nchi bila kuwategemea wao, Anaonekana kuwa ni tishio kwa siasa za Magharibi, hivyo mabeberu wameungana kwa nguvu zote kuona kuwa Uchaguzi huu uwe na maslahi kwao, lakini inyeshe mvua, lije jua Magufuli atashinda mapemaaa.
 
Sasa fikiria nguvu waliyotumia mataifa ya magharibi dhidi ya taifa hilo waielekeze Tanzania. Tutatoka salama kweli?
Hatuwezi kutoka mkuu, hizi nchi zetu hata Kama tukikomaa na misimamo yetu madhara ya kiuchumi yatakuwa makubwa sana, na kuepuka hata umoja wa kitaifa na uzalendo wa nchi ni kitu muhimu Sana, dhuluma na uonevu utawapa watu sababu ya kutuvamia kutoka nje
 
Sisi wanatuvutia muda sababu hatuna affect kwao
 
CCM chama tawala milele au nimekosea wanazengo?
 

Ni kweli kabisa lengo la USA ndilo hilo - lakini mimi siamini kama Uncle SAM atafakiniwa katika crusade zake za kutaka kuisambaratisha Urusi au kuishambulia kijeshi - Majenerali wa jeshi la USA wakijaribu kutekekeza upuuzi huo,basi, huo ndio utakuwa mwisho wa Amerika ya Kasikazini, ukweli huo wanaujuwa vilivyo wakuu wa Majeshi ya Merikani, historia inaonyesha hakuna Taifa lolote/majeshi yalio wahi kuivamia/shambulia Urusi na likabaki salama bila ya kusambaratishwa na majeshi ya Urusi.

Kitu kingine hivi sasa ushirika wa NATO hupo mashakani, miaka ya karibuni hasa baada ya Trump kuingia madarakani Ushirika huo umeanza kuonyesha nyufa za hapa na pale, mfano: Taifa la Uturuki kukataa ushauri wa Merikani kwamba wasinunue S-400 air defense system kutoka Urusi, Uturuki ilipuuzia ushauri wa Merikani wakanunua S-400 integrated air defense system - hilo la kwanza, la pili ni pendekezo la Ufaransa na Ujerumani la kutaka washirikiane katika uundaji wa ndege za kivita na kuachana kununua ndege za vita kutoka Merikani.

USA ilitaka kuzorotesha viwanda vya kuunda silaha na ndege za vita vya huko Ulaya ili Continental Europe iwe tegemezi kwa silaha kutoka Merikani, njama hizo Ufaransa, Ujerumani na Italy walisha zishtukia - la tatu ni pendekezo la Ujerumani kwamba Mataifa ya Ulaya yawe na jeshi lake independent pendekezo hilo linadhilisha kwamba Mataifa hayo yamekwisha choshwa kuburuzwa na Merikani kwenye adventures zake zisizo kuwa na kichwa wala miguu.
 
Wanaweza kumtambua Lisu kama mshindi kwenye uchaguzi huu ili kuleta mabadiliko ya kimfumo ndani ya taifa hili lenye historia ya kutawaliwa na chama kimoja kwa muda mrefu
Chama kimoja kwa muda mrefu? Nilidhan labda utasema mtu mmoja kwa muda mref
 
Japo huwa siwapendi westerners Ila huyu luka-shenko msambaa wa beralus Ni mchimbachumvi sana
 
Hawawezi kutumia hiyo nguvu kwa kuwa hatuna mawese.
Watatumia kwa sababu ya kumdhibiti China anae onekana kuwekeza nguvu zake nyingi Afrika kwenye masuala ya kiuchumi na sasa anataka kuwekeza kijeshi. Hilo NATO hawatakubali lifanikiwe
 
Unalichuki taifa ambalo limekupita kila kitu ni ujinga mtupu na huyo huyo putin amemuomba akubari kuitisha uchaguzi mwingine. Hivi kwa akili yako unadhani bila marekani na huko uraya magharibi hii Dunia ingetawarika
 
Hiyo mikopo aliyokopa hadi akavunja rekodi ya marais wote waliomtangulia ameikopa wapi, CRDB au NMB.

Kwa akili zako hizo kidogo ulizo nazo unafikiri Magufuli anaweza kuitawala hii nchi bila kutegemea chochote toka nje!!

Wewe ndio kabisa hata hujui unachoongea afadhali hata ukae kimya tu.
 
Bahati mbaya Venezuela Nicolas Maduro wananchi walikua wanamtaka.Guaidado alikua akifosi tu.Ila Lukashenko amefanya big violation of human rights na kavunja kabisa democracy.
 
Bahati mbaya Venezuela Nicolas Maduro wananchi walikua wanamtaka.Guaidado alikua akifosi tu.Ila Lukashenko amefanya big violation of human rights na kavunja kabisa democracy.
Ni kweli ila hata Belarus mambo yatakuwa sawa sababu purtin keshamkingia Alexander Lukashenko kifua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…