Belarus kujaribu kuokoa jahazi la Urusi, yatoa msaada

Belarus kujaribu kuokoa jahazi la Urusi, yatoa msaada

Mrengwa wa kulia

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2022
Posts
1,091
Reaction score
3,695
Wafuatiliaji wa shughuli za kijeshi wamesema kwamba rais wa Belarus Alexander Lukashenko anatoa msaada wa kijeshi na silaha kwa Russia katika vita vinavyoendelea Ukraine.

Belarus imeruhusu karibu wanajeshi wa Russia waliosajiliwa hivi karibuni kupokea mafunzo nchini humo, huku ikitoa karibu silaha nzito 211 kwa Russia.

Kiongozi wa upinzani Sviatlana Tsikhanouskaya ameambia VOA kwamba rais Lukashenko anaendelea kutoa msaada kwa Rafiki wake mkubwa, rais wa Russia Vladimir Putin.

Tshikhanouskaya amesema kwamba Lukashenko anatumia msaada huo kama mkakati wa kisiasa kuendelea kukaa madarakani na kutaka kuonyesha kwamba ni mwaminifu kwa Putin.

Russia imekuwa ikitumia Belarus kupanga mashambulizi dhidi ya Ukraine.

Wafuatiliaji wa shughuli za kijeshi nchini Belarus, ikiwemo Hajun, wamesema kwamba idadi ya wanajeshi wa Russia nchini Belarus inaendelea kuongezeka na kuna ripoti kwamba kambi za kijeshi za Belarus zina idadi kubwa ya wanajeshi kuzidi kiasi na kwamba Russia imeanza kujenga kambi mpya ili kuendelea kutuma nchini humo wanajeshi zaidi.

Chanzo: VoA

UKRAINE ANAPAMBANA NA MATAIFA MAKUBWA ZAIDI YA 10.
 
Mpaka sasa bado hainingii akilini kwa Urusi niliyodhani naijua ndio hii inatapata na kuteswa na kainchi kadogo, inakaribia mwaka mmoja sasa.
Hata mimi siielewi hii ni Urussi gani inayohaha kiasi hiki hadi kuomba misaada kutoka Belarus, Iran, N.Korea, Kampuni binafsi ya Wagner, Inakamata wanafunzi wa Kiafrika na kuwalazimisha kuingia vitani, n.k. Yan Urussi sasa imekuwa one among the inferior and powerless countries.
 
URUSI haitaki kueleweka na watu wengine wakijielewa wenyewe inatosha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom