sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Nchi ya Belarus inatmua maharamia kuidhofisha EU ikiwa na lengo la kujaza maharamia wengi sana kwa kuwasaidia kuzamia katika nchi za EU.
katika miezi ya hivi karibuni, maelfu ya watu wamesafiri kwenda Belarus kutoka Mashariki ya Kati, Afrika na Asia ili kuzamia Ulaya ya magharibi. maharamia wamesaidiwa na serikali ya Belarus kwa kutumia kampuni za watalii zinazotoa vibali, kampuni hizo ziliwapangia safari za ndege hadi Minsk mji mkuu wa Belarus na kutoa usafiri wa ardhini hadi mpakani mwa Poland. Mara baada ya kufika huko,wanajeshi wa Belarus huwaonyesha mahali palipo mpaka wa kuingia Poland na kisha kuwazuia kurudi .
Pia raisi wa Belarus kachimba biti kwamba, bomba la gesi inayotumika na nchi nyingi za EU, linapita kwenye nchi yake kwa hio akiwekewa vikwazo anaweza kupiga blok hio gesi na kuwalaza na baridi.
huko mpakani mwa Poland hali si hali, mda wowote inaweza kunuka