Mwadilifu Mdhulumiwa
JF-Expert Member
- Jul 22, 2021
- 419
- 640
Wandugu Salamu!
Niende moja kwa moja kwenye mada.
Nikiwa kama mdau wa soka na shabiki wa Club ya Simba nimefanya ufuatiliaji wa performance ya kikosi chetu, nimebaini aadhi ya mapungufu ambayo kwa namna moja au nyingine yametunyima ushindi katika mechi tatu muhimu tulizocheza hadi sasa.
Ukiacha ile mechi ya tarehe 19 tuliyopoteza dhidi ya Mazembe, Ile game na Yanga kwakweli hatukupaswa kupoteza maana ilisababisha tuvuliwe taji la ngao ya jamii, wakati sare na Biashara imetufanya kupoteza point 2 muhimu na hivyo tukijikuta sasa tunajipa kazi nyingine ya kuwaombea njaa washindani wetu ili kuja kukamata usukani wa ligi.
Kasoro nilizoziona katika benchi la ufundi na kikosi cha Simba ni hizi zifuatazo:-
Kufanya Sub kwa Mazoea
Ukiacha ile mechi tuliyocheza na Mazembe ambapo ilikuwa muhimu kuwabadilisha wachezaji ili kutoa nafasi kwa mashabiki kuwaona mastaa wote tuliowasajili msimu huu, Lakini kwa ile mechi Yanga, benchi la ufundi lilifanya kitu cha hovyo kumtoa Dilunga na kumuacha Mugalu wakati mle ndani Dilunga alikuwa bora zaidi ya Mugalu.
Lakini kilichoonekana ni kwamba tayari ilikuwa imeshapangwa kuwa kipindi cha pili Dilunga atampisha Boco, lakini kabla ya kufanya hili ilitakiwa benchi la ufundi liangalie kwa umakini nani alitakiwa kutoka kati ya Mugalu na Dilunga?
Sikuona kabisa sababu ya kumuacha Mugalu aendelee na kipindi cha pili, hapa naliomba benchi letu la ufundi wawe wepesi wa kufanya mabadiliko ya kikosi kabla mtu hajavurunda zaidi.
Tatizo hili pia limejirudia hata kwenye mechi na Biashara United, Kagere tayari alionekana kuishiwa mbinu toka kipindi cha kwanza kutokana na mabeki kumkamia kupita kiasi, Hivyo bench la ufundi walipaswa kumuingiza Sakho tangu Dakika ya 46, nafikiri sote ni mashahidi tuliona jinsi SUB ya Sakho ilivyoleta mapinduzi kwenye safu ya ushambuliaji baada ya kumbadili Kagere. Ni Sakho huyo ndiye alisababisha tukapata ile muhimu ambayo hata hivyo umakini mdogo wa Boco ukatuangusha.
Nashauri sana Boco asiruhusiwe tena kupiga penati kama timu haijashinda. Mimi tangu Boco akose penati kwenye ile mechi na Nkana kule Zambia mwaka 2018, nilishampigia mstari mwekundu, maana siuonagi ufundi anaoutumia kufunga zile penati anazofunga. Fundi wa kupiga penati Simba ni Elasto Nyoni na alikuwemo kikosini!
Narudia tena Boco asipige tena penati labda samba iwe iwe imeshashinda!