Benchi la ufundi Ihefu FC, msitufanye mashabiki hatuna akili tunajua kila kitu kinachoendelea nyuma ya pazia

Benchi la ufundi Ihefu FC, msitufanye mashabiki hatuna akili tunajua kila kitu kinachoendelea nyuma ya pazia

Ndiyoooo, Sina muda wa kutoa salamu maana nitakua napoteza muda tu, twende moja kwa moja kwenye point kuu.

Hakika NALIA NGWENA toka nianze kushuhudia mpira sijawahi kushuhudia robo fainali mbovu Kama hii ya simba vs ihefu huu ni ukweli usiopingika.

Hii siyo ihefu iliyoifunga yanga, Wala siyo ihefu iliyoifunga Azam na wala siyo ihefu iliyokuja kuleta changamoto uwanja wa mkapa kwa wakubwa wa kariakoo.

Nilitegemea kuona mpira wenye ushindani mpira mzuri na wakuvutia na nilitegemea kuona mpaka dakika tisini hakuna goli ni mwendo wa matuta.

Benchi la ufundi ihefu fc, jitafakarini kwa hicho mlichokifanya nyuma ya pazia ili kuwapa unafuu hao wakongwe wa kariakoo, ni Jambo la kusikitisha sana Simba anaingiza timu yake ya kikosi Cha kwanza halafu kocha wa ihefu unaingiza kikosi Cha mazoezini.

Lazima utakula nyingi tu, kocha wa ihefu siyo mgeni na timu za kariakoo ila ulichokifanya ni makusudi kwa sababu kilichopo nyuma ya pazia unakijua na ndiyo maana ukaamua kuingiza wachezaji wasiojua hata kutuliza mpira.

My take, kwa hali hii mpira wetu wa Tanzania utakua unapiga hatua mbili mbele Kisha kurudi hatua tano kuja kujipongeza.
Bwanako hajakusaliti acha wivu

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Na hizi ni njama za mwamedi amempa bahasha fahadi...nampigia fady anacheka tu et "kaka mpira una matokeo matatu" yaani kirahisi kabisa ananijibu mimi hivyo kundulake

ndio maana wahindi siwaamini kabisa
Ujanja ujanja mwingi hakuna Radha ya mpira kabisa.
 
Jitahidi utumie paracetamol inapunguza maumivu, sema usizidishe 4grams kwa siku unajiweka katika hatari ya kupata magonjwa ya ini ambapo utapata kitambi cha maji.
 
Tupe record za ihefu vs simba ktk mashindano yt ktk misimu 2 hii ..
 
Jitahidi utumie paracetamol inapunguza maumivu, sema usizidishe 4grams kwa siku unajiweka katika hatari ya kupata magonjwa ya ini ambapo utapata kitambi cha maji.
Sawa Daktari nasikia huwa zinaongeza na umbumbumbu Kama wako.
 
wamepigwa khamsa ihefu, linalalamika shabiki la utopolo.

ukisikia mchezo wa mpira una baadhi ya mashabiki vichaa, ndio kama hivi.
 
Mimi ni simba
Hisia zangu naona tumekopwa ushindi sisi tutawapa wa ligi sababu ligi hatuna tunachopambania
Nasubiri game ya ligi nijiprove wrong
 
Nyie yanga mlipokula 4 kwa 1 mlikuwa mmefanya nini?

Ukianza kumlaumu ihefu jiulize wewe ktk hatua hii kipi kiliwahi kukukuta.
 
Nyie yanga mlipokula 4 kwa 1 mlikuwa mmefanya nini?

Ukianza kumlaumu ihefu jiulize wewe ktk hatua hii kipi kiliwahi kukukuta.
Sawa ngoja wydad aje mumpige hizo tano mnazoziita hamsa.
 
Back
Top Bottom