kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Taifa stars ifundishwe na walimu wenye ubora na uzoefu mkubwa kuliko wachezaji wanakotoka kwenye timu zao. Hii itachechemua fikra za wachezaji kuhusu timu yao ya Taifa. Mwanafunzi wa chuo kikuu kufundishwa na mwalimu wa secondari haiamshi hamasa ya mwanafunzi kutaka kujifunza. Timu yetu ya Taifa inafundishwa na walimu wenye CV na uzoefu hafifu sana wa mechi za kimataifa, hatutoboi hata kidogo kama tutaebdelea hivi.
Sio tu wachezaji lakini hata mashabiki hawako tayari kwenda kuona timu inayofundishwa na kocha ambae hana uzoefu wa kuifikisha timu hata nafasi ya nne za juu kwenye ligi ya nchi yoyote duniani. Timu inafundishwa na makocha wa low profile kuliko makocha wa timu za wachezaji, hii inaleta mtafaluku kwenye kikosi, hakuna nidhamu au kunakuwa na nidhamuya woga tu ya wachezaji kuogopa bifu na visilani vya kutokuitwa timu ya taifa.
Lazima tupate mwl ambae amewahi kuifikisha timu kwenye nusu au finali au kuchukua kombe la Afcon, CAF au world cup, sio vinginevyo.