Benchi la ufundi Simba

kwa kifupi simba hatuna kocha. sub aliyofanya ndio imeuwa game. morrison alivyotoka ilitakiwa kocha atake advantage. boko ndio alitakiwa kutoka na kuingia kanda. kanda na kahata wangeenda pembeni na kagere kati. yanga baadae walirudi nyuma sana na ndio maana mkude ali relax. sasa jamaa alichokifanya analijua mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sven na Aussems wote hawajui kubadili mbinu uwanjani, wanacheza namna moja wakati wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Humjui Aussems; mechi Simba anamtoa Nkana uwanja wa taifa, alifanya sub akamuingiza Dilunga alieenda kutoa assist kwa Chama aliefunga goli la tatu tukawatoa wale jamaa.

Na sio mechi hiyo tu, Dilunga alitumika sana na Aussems kwenda kuzimaliza kipindi cha pili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
simba haijawahi kuwa timu bora ukiacha viongozi kina manara kuhonga marefarii pamoja na kumwagia upupu vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji. Kina manara wanamdanganya mo wamlie hela zake. Alipotishia kuwafukuza baada ya mapinduzi cup ndio kasi ya marefa kuharibu mechi za simba ilipoanza. viongozi wa simba wanajua nini kinachoendelea, mbumbumbu watabaki kulaumu tactics, simba hamna kitu pale

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati mwingne unatakiwa kukubari marokeo na kumheshimu mpinzani,

Ukweli ni kwamba yanga walituzidi kimbinu

Matokeo ya

Simba Vs Yanga

R. Madrid Vs Barça

Man Utd Vs Man City

Zote hizo zimeamuliwa kimbinu na bahati pia lakini haina maana Team zilizoshinda ni bora kuliko zilizofungwa....


Ukiona huna uwezo wa kubeba ubingwa basi mkamie bingwa , shinda, then maisha ya kila siku yaendelee.. [emoji23][emoji23][emoji23]

Bado naliamini bench la Ufundi

Simba tupo vizuri, usajili utakaofanyika wajikite kwenye ulinzi na washambukiaji


Bocco na Kagere wanapaswa kuwa na changamoto

Hongereni Watani mlituweza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mapungufu ya benchi hasa kimbinu kwa head coach wa simba yapo wazi , labda kama sio mfuatiliaji wa mpira
Sio kweli, mnamcriticize kocha kwenye game zinazokuwa tofauti na matarajio yenu ,Kwa mfano mechi ya Mapinduzi dhidi ya Mtibwa na draw ya 2-2 dhidi ya Yanga mlimsema sana kocha, akashinda game kadhaa katikati hapa mkasahau ubovu wake kiujumla, mkaanza kujimwambafai eti "mtatueleza ile droo mliipataje", leo kafungwa kawa mbaya tena [emoji16][emoji16][emoji23]
 
Matola hawez kuwa headcoach... Leseni yake hairuhusu
Sent using OnePlus 6T Maclaren Edition
 
Namjua Aussems kuliko wewe, tulikuwa tunakwenda Misri na Kongo klabu bingwa Afrika tukiwa tumefunguka kabisa na matokeo yake unayajua.

Kocha mwenye akili hawezi kwenda ugenini akacheza staili ile ile inayocheza nyumbani.

Ndio maana tulimfukuza hana mbinu kama mbelgiji mwenzake Sven.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo sahihi kabisa mkude alipaswa kuwa na msaidizi pale Kati, kutokuwepo kwa Mzamiru Yasin ni tatizo kubwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…