Benchi la ufundi Simba

Benchi la ufundi Simba

Hivyo vichezaji vyenu vyote japo vinarukaruka tu. Ajib+mmakonde+ mkude+ chama+kahata= Balama Mapinduzi. Usimguse kabisa Haruna
Hao wachezaji kama wangekuwa kama Balama Mapinduzi wasingekuwa wanaongoza ligi. Na kama Mapinduzi angekuwa kama hao wachezaji Yanga ingekuwa inaongoza ligi.

Huyo Mapinduzi Balama mbona hatukumuona mlipocheza ma Mbeya City.

Balama ajiandae kucheza mchangani, kimataifa asahau maana hata FA Yanga hawachukui.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu,

Ni muda mrefu sasa nina mashaka na uwezo wa benchi la ufundi la Simba. Hata ushindi tunaopata ni juhudi binafsi zaidi kuliko maelekezo ya kiufundi.

Mechi ya leo ni mfano bora kabisa. Huwezi kuanza kwa kumtumia kiungo kama Kahata ambaye anacheza staili inayofanana na viungo wa Yanga! Mechi ya leo ilihitaji viungo wenye kasi zaidi.

Hata timu inapoonesha kulemewa hakuna mabadiliko ya haraka! Timu inacheza vile vile wakati plan zimeshafeli. Mkude alihitaji msaidizi wa kukaba sababu ya staili yake ya uchezaji lakini kumpanga na watu slow na wasio wakabaji kama Kahata na Chama ilifeli mapema toka mechi ianze na kulikuwa na hatari ya kupata hata kadi nyekundu ilipaswa benchi la ufundi ku change plan haraka!

Simba ina chief coach ambaye hana experience na kufundisha club zaidi ya kupatia experience Simba. Wachezaji wanatoa kila walichonacho lakini plan mbovu kwa mechi za kimbinu kama hizi zinawaangusha.

Simba ina timu bora kabisa, tunahitaji pia benchi la ufundi bora ili kitumia vipaji vilivyopo vizuri.

Nimeandika hili baada ya kufatilia mechi nyingi zaidi ya mechi ya leo na pengine ushindi hututia upofu lakini zipo mechi nyingi makocha wa timu pinzani wanafanikiwa kimbinu lakini wanazidiwa na experience ya wachezaji wa Simba kimbinu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pamoja na maoni yako mazuri ya kitaalam, lkn hii mechi Simba walishindwa kabla ya kuingia uwanjani. Kosa kubwa lilifanywa na TFF aidha Kwa makusudi au Kwa kutokujua au Kwa kutokujali. Makosa ya timu ni madogo ingawa yapo. Nitaeleza kidogo.

Duniani pote inapofika mechi ngumu kama hizi Derby za watami au Ile el clasico ya Hispania, timu zinapewa muda mzuri wa kujiandaa si chini ya wiki moja. Zikilazimika kuchezea mechi kabla ya mechi za Derby, zitacheza na timu za kawaida kabla ya hizo Derby.

Safari hii ktk hali ya kushangaza, siku tatu kabla ya mechi ya watani Simba ilipangwa kucheza na Azam moja ya timu ngumu Tanzania Kwa sasa. Waliofuatilia mechi Ile ilikuwa ngumu sana na Simba ilishinda Kwa mbinde. Kitendo cha kufuatiwa na mechi nyingine ngumu kama ya Yanga, kuliwachosha wachezaji sana Kwa kuwa almost timu ilikuwa Ile Ile iliyocheza na Azam.

Kwa hiyo Simba walizidiwa na wachezaji walikuwa wamechoka. Kama Yanga ingejipanga vizuri ingeweza hata kushinda Kwa goli tatu.
Mengine madogo mi timu kujiamini kupita kiasi na kudhani Yanga ni wanyonge. Hili lilichangia Kwa sehemu ndogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakuunga mkono,fraga alitakiwa kuanza sababu anajua kunusa hatari na mtu wa kutumia minguvu kama viungo wa yanga,simba inacheza kibishoo sana na kwa style hiyo itachukua muda sana kuifunga yanga sababu yanga wakicheza na yanga wanacheza kufa na kupona kitu ambacho simba hawana kasi hiyo,fraga anakaba sana katika viungo wa simba anatakiwa kuanza mechi nyingi
Kuna watu ukiwaambia wanabisha fraga no binge la mchezaji Yuko kikazi zaidi anaziba njia hakai na Moira ikitokea nafasi anafunga mkude yupo kibishoo zaidi siyo mkude wa miaka minne iliyopita
 
Pamoja na maoni yako mazuri ya kitaalam, lkn hii mechi Simba walishindwa kabla ya kuingia uwanjani. Kosa kubwa lilifanywa na TFF aidha Kwa makusudi au Kwa kutokujua au Kwa kutokujali. Makosa ya timu ni madogo ingawa yapo. Nitaeleza kidogo.

Duniani pote inapofika mechi ngumu kama hizi Derby za watami au Ile el clasico ya Hispania, timu zinapewa muda mzuri wa kujiandaa si chini ya wiki moja. Zikilazimika kuchezea mechi kabla ya mechi za Derby, zitacheza na timu za kawaida kabla ya hizo Derby.

Safari hii ktk hali ya kushangaza, siku tatu kabla ya mechi ya watani Simba ilipangwa kucheza na Azam moja ya timu ngumu Tanzania Kwa sasa. Waliofuatilia mechi Ile ilikuwa ngumu sana na Simba ilishinda Kwa mbinde. Kitendo cha kufuatiwa na mechi nyingine ngumu kama ya Yanga, kuliwachosha wachezaji sana Kwa kuwa almost timu ilikuwa Ile Ile iliyocheza na Azam.

Kwa hiyo Simba walizidiwa na wachezaji walikuwa wamechoka. Kama Yanga ingejipanga vizuri ingeweza hata kushinda Kwa goli tatu.
Mengine madogo mi timu kujiamini kupita kiasi na kudhani Yanga ni wanyonge. Hili lilichangia Kwa sehemu ndogo

Sent using Jamii Forums mobile app
Viongozi wa Simba no mbumbumbu na yaani wwanakaa kimya Kama yatima wapowapo tu
 
Simba kufungwa na Yanga si kitu cha ajabu kwa sababu mpira unadunda. Na watu wengi wanaowalalamikia ni kwa sababu hawaujui mchezo wa mpira kiundani. Na siku hizi tangu ligi za ulaya na hii ya bongo ziwe zinaonyeshwa kwenye TV kila mtu kawa kama sio kocha basi mchambuzi wa mpira. Barca kafungwa na Madrid, Liver kapigwa na Watford na hapa hao mashabiki wanasemaje?

Simba pamoja na kufungwa na Yanga bado ni timu nzuri na ina uwezo wa kuchukua kombe la ligi na FA kwa pamoja. Mapungufu yaliyopo ni madogo madogo sana na kwenye mchezo wa "derby" yeyote anaweza kufungwa bila kujali ubora timu iliyonayo.

Kuna watu wanamlaumu Manula kwenye faulo aliyofungwa lakini hawautaki ukweli mchungu wa kumpongeza mpigaji wa ile faulo. Hakuna kipa duniani aliyekamilika kwa asilimia 100 duniani. Ni kweli mapungufu ya Manula yapo kwenye kona, krosi na mipira ya kutenga. Lakini kwa mtizamo wangu ni mapungufu ambayo ameyapunguza kwa asilimia kubwa kwa siku za karibuni. Lakini kwa hili Simba inapaswa imuangalie kwa jicho la tatu kocha wa magolikipa. Je ana elimu, uwezo na uzoefu wa kutosha kuwafundisha magolikipa wa timu kubwa kama Simba? Je ushauri wa Ausems kabla ligi haijaanza Simba ilitakiwa iwe na kocha mwingine wa makipa ulifanyiwa kazi kwa kiasi gani na uongozi wa Simba? Kwangu mimi Manula bado atakuwa namba moja Tanzania kwa kuokoa yale mashuti ya uso kwa uso pale kipa anapokutana na washambuliaji. Hayo mengine ya krosi na kona yanarekebishika Simba ikipata kocha sahihi wa makipa.

Kwa wale wanaolaumu Mkude wanapaswa waulaumu uongozi wa Simba kwa kumuuza Kotei na pia walilaumu benchi la ufundi kwa kutompanga Fraga sambamba na Mkude kwenye mechi ngumu. Mkude sio mzuri sana kwenye kupokonya mpira ndio sababu Ausems alikuwa anapenda kuwatumia Mkude na Kotei/Mzamiru kwa pamoja kwenye mechi kubwa. Mkude ni Mzuri zaidi anapokuwa na mpira yeye miguuni mwake lakini adui yake akiwa na mpira utamuona Mkude kiungo wa ovyo kabisa.

Kwa wengine wanamlaumu Chama eti yupo "slow". Kama kuna mchezaji timu pinzani hazipendi kukutana naye ni huyo Chama. Kiukweli yupo taratibu lakini sio wakati wote. Mwangalie sana wakati wa kushambulia anavyoongeza kasi yake kwenda mbele na pasi za mwisho anazotoa. Kinachomuangusha kwa sasa ni washambuliaji wanapoteza sana pasi zake za mwisho. Huyu kwangu ni "slow but sure"

Boko na Kagere kwangu bado ndio fowadi bora kabisa kwenye VPL. Tatizo ni umri wao na kucheza mechi za ligi mfululizo. Hapa walaumiwe viongozi wa Simba. Tuliwashauri sana hapa jamvini kabla ya msimu kuanza waongeze mshambuliaji wa kuwasaidia hawa wazee wetu mafundi wa kutupia. Matokeo yake wakamleta mbrazil Wilker. Wakati wa dirisha dogo walipomuacha Wilker tukashauri waongeze mshambuliaji asili wakati hata mtanzania tena tukaenda mbali zaidi tukawataja wakina Paul Nonga, Saliboko, Kibaya n.k. lakini viongozi wao wakawaongeza mawinga/wasaidizi wa washambuliaji Luis na Kichuya. Japo nawapongeza kwa Luis maana ile ni mashine kubwa lakini nafasi ya Kichuya ilipaswa aongezwe mshambuliaji asili ili kuwe na mapumziko kwa wazee wetu wa kazi Kagere na Boko. Boko na Kagere wana uwezo wa kucheza na kufunga sana tu hata misimu mitatu ijayo iwapo tu wataongezewa washambuliaji vijana wawili mmoja awe kutoka nje na mmoja atoke hapa Tanzania kwa sababu watakuwa na muda mrefu wa kupumzika tofauti na sasa ambapo wanacheza mechi mbili kila wiki na hawana watu wa kubadilishana nao.

Beki za kati kwa sasa pale Simba ni janga hasa baada ya Erasto kuwa na maumivu ya mara kwa mara. Ila kiukweli kwa msimu huu iwapo ule upuuzi wa kutaka kumuacha Wawa ungefanyiwa kazi wakati dirisha kubwa la usajili kwa kweli hata ubingwa Simba ingeusikia tu. Pamoja na Wawa kuwa na mapungufu kwenye krosi na kona lakini yeye ndio kaibeba Simba yote pale katikati bila yeye sijui Simba ingekuwa nafasi ya ngapi kwenye msimamo wa ligi.Uzoefu wake na nguvu alizonazo vimeisadia sana Simba msimu kwenye ligi ya ndani. Kwangu mimi anastahili msimu mmoja au hata nusu msimu tena wakati mabeki wapya watakapokuwa wanaingia kwenye mfumo wa Simba.
 
Kuna watu ukiwaambia wanabisha fraga no binge la mchezaji Yuko kikazi zaidi anaziba njia hakai na Moira ikitokea nafasi anafunga mkude yupo kibishoo zaidi siyo mkude wa miaka minne iliyopita
Kinachonishangaza inakuwaje mtu kama Matola hali akiijua vizuri Yanga inavyocheza kwa nguvu na kasi akaacha kumpanga kiungo mkabaji nyuma ya Mkude.

Matola amecheza Simba muda mrefu na anaijua falsafa ya Yanga nini kilimfanya ajichanganye hivyo, au kocha anampuuza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulishasema Simba ina kocha mwenye experience ndogo. Hata wachambuzi wetu wengi hawaoni hilo. Simba haifanyi vizuri kimbinu zaidi ya uwezo binafsi tu. Tunahitaji kocha mwenye experience na soka la Africa otherwise champions league hatufiki popote tukikutana timu bora.
 
Udhaifu ule ule no urgency na mbinu hazibadiliki. Angalia Kaze alivyoibadili Yanga hadi Kaseke ana deliver vipi angekuwa na Konde boy?
Hakika mkuu. Tactically coach wa simba ana mapungufu mengi sana. Ukitazama mechi zote ambazo simba anakutana na wapinzani wenye kupush timu inakuwa haina utulivu, No urgency,. Unamuacha chama anacheza dk 90, huku unaanza na kiungo mkabaji mmoja...poor game plan
 
Kinachonishangaza inakuwaje mtu kama Matola hali akiijua vizuri Yanga inavyocheza kwa nguvu na kasi akaacha kumpanga kiungo mkabaji nyuma ya Mkude.

Matola amecheza Simba muda mrefu na anaijua falsafa ya Yanga nini kilimfanya ajichanganye hivyo, au kocha anampuuza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Matola asilaumiwe yy ni mshauri tu kwa Sven Mie nadhani uongozi utoke useme kwani kocha akiharibu ataondoka na si ajabu akajiunga na wapinzani wetu hao hao anaowapa unafuu leo kwenye upangaji timu sie hatuna pa kwenda
 
Hivi Bwaliya ameuzwa? Maana simuoni wala kumsikia. Mechi ya jana hali ilikuwa tete, tumshuru refa alikuwa nyuma ya tukio hakuona vizuri akatoa penati. Ila bench la ufundi linahitaji mbadala
 
Hivi Bwaliya ameuzwa? Maana simuoni wala kumsikia. Mechi ya jana hali ilikuwa tete, tumshuru refa alikuwa nyuma ya tukio hakuona vizuri akatoa penati. Ila bench la ufundi linahitaji mbadala
Bwalya yuko Zambia ana matatizo.. ngoja LWANGA azame ndani usajili mpya
 
Mo utashtuka tupo nje champion league na VPL ubingwa rehani
Nahisi Mo anapenda makocha wa bei rahisi kwa timu inayotaka bora afrika lazima awekeze kwenye benchi la ufundi.
Ni afadhali uwe na wachezaji wa kawaida lakini uwe na kocha bora kuliko kuwa na wachezaji bora lakini kocha bomu
 
Ni kawaida team kutamba kwa uwezo wa wachezaji Binafsi,IPO exceptional moja tu ya Ajax class of 1992.Brazil iliinuliwa na Kina Zico, Socrates, Garincha, Pele, Tostao,Romario,Bebeto,Ronaldinho,De Lima,Kaka, Argentina Class of 1986 iliinuliwa na Maradona, Barcelona iliinuliwaga na kina Johan Cruyff, Ronaldinho,Xavi, Iniesta na Messi, Real Madrid iliinuliwa tangu kale na Kina Ferenc Puskas na Alfredo De Stefano na Ronaldo.Wala sio Dhambi team kuinuliwa na viwango binafsi.kwa mpangilio wa hoja zako INA maana vikosi vyote hivyo vilikuwa na Makocha Wabovu???
 
Brazil ya 98 na 2006 ilikuwa na vikosi bora lakini haikubeba kombe sababu makocha wao walikosa mbinu za ziada
 
Back
Top Bottom