Benchi la ufundi Yanga sc, nadhani mmeona dharau alizozionesha Benard Morrison kwenye mchezo wa Yanga dhidi ya Dodoma jiji Fc

Benchi la ufundi Yanga sc, nadhani mmeona dharau alizozionesha Benard Morrison kwenye mchezo wa Yanga dhidi ya Dodoma jiji Fc

Nianze kwa kutoa pongezi zangu za dhati kabisa Tena kwa moyo mkunjufu kwa Yanga sc kutwaa ubingwa /kuchukua kombe la Nbcpl kwa Mara ya ishirini na tisa (29).

Hakika pongezi hizi zifike kwa viongozi wa simba, ooh kumradhi viongozi wa Yanga sc , benchi la ufundi pamoja na mashabiki hakika hakika mnastahili sifa.

Twende moja kwa moja kwenye maada Kama kichwa Cha habari kinavyojieleza.

NALIA NGWENA, nilishitushwa kidogo kuona Benard Morrison (Toto tundu) kufanyiwa "sub" lakina hakutaka kutoka na huku aliyetakiwa kubadilishana naye (Clement mzinze) alikua tayari kasimama na alisimama nje kwa dk tano (5).

Mpaka mashabiki walipoanza kumzomea Morrison ndipo akatii wito wa kutoka nje na Clement mzinze akaingia.

Kimtazamo huu ni utovu wa nidhamu, Prof Nabbi hakutaka kumpa hata mkono na Morrison alikwenda benchi hakutaka hata kuwapa mikono wachezaji wenzake.

Sub ya Clement mzinze ilikwenda kuzaa matunda nakupata goli la kusawazisha.

Morrison hastahili kuwa Yanga msimu unaokuja, utoto wa namna hii na ujinga utakuja kuigharimu timu.
Naunga mkono hoja. Kama viongozi wa Yanga watakosa kabisa mbadala wake mwenye ubora wa hali ya juu, basi ni bora tu wakamrejesha Yacouba Sogne kutoka Ihefu!

Ila siyo Bernard Morrison, ambaye kiukweli mchango wake umebakia kuwa mdogo sana katika timu yetu.
 
Morrison anajua mpira ila sijui kama yupo sawa kichwani yeye hata kupata kadi yeyote kwenye mechi muhimu haoni tabu kwa wale Wydady wanaotengeneza mazingira ya Kadi nyekundu kama walivyofanyiwa Mamelodi jana huyo Morrison achukui hata dakika kadhaa anatengenezewa mazingira ya nje ili wapate ushindi kirahisi...
 
Kweli kabisa mkuu anahitajika mchezaji mwenye talanta na nidhamu siyo huyo mwenda wazimu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Morrison anajua mpira ila sijui kama yupo sawa kichwani yeye hata kupata kadi yeyote kwenye mechi muhimu haoni tabu kwa wale Wydady wanaotengeneza mazingira ya Kadi nyekundu kama walivyofanyiwa Mamelodi jana huyo Morrison achukui hata dakika kadhaa anatengenezewa mazingira ya nje ili wapate ushindi kirahisi...
Huyo dogo hawezi kubadilika kabisa huyo ni sikio la kufa.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sawa boss, na moloko akipatikana winger mzr na mwenye kasi na yeye atupishe....kwa heshima tutawaaga, na huyu feisal aombe samahani then tuendelee kushehekea ubingwa msimu ujao
Wampe kibunda Pro Nabbi achague wachezaji anaowataka yeye hakika tutaona mzuri kutoka yanga.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Tanzania mchezaji akifunga kwenye mechi ya simba na yanga tu basi basi hata afanye ujinga gani watu hawana mda nae na juzi katoka kufunga kwenye kombe la looser akichukua goal lake mngeshinda kweli ile mechi.
 
Back
Top Bottom