Benchikha hana meno hapo Simba, hajazoea mpira wa kubembelezana

Benchikha hana meno hapo Simba, hajazoea mpira wa kubembelezana

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Benchikha alipokuja tu Simba, niliwahi kuja na nyuzi mbili nikitoa tahadhari kuwa mafanikio yake yanaweza kuwa duni kutokana na hali aliyoikuta Simba. Kwanza niliongelea suala la quality ya wachezaji aliopewa aende nao vitani. Pili nikaja kuongelea athari za kurithishwa migogoro kati ya wachezaji na viongozi ambayo yangeathiri utendaji wake wa kazi.

Yote niliyoyasema yameenda kutimia. Benchikha ameachwa amtegemee Ntibazonkiza kwa kile kinachosemekana na wengi kuwa mkataba wake unamlazimisha kumtumia. Kama hiyo haitoshi akanyang'anywa kina Phiri akaletewa kina Freddy. Leo hii eti watu wanasema kocha hana mbinu za ushindi. Yale yale ya siku zote kumuangushia kocha jumba bovu ili wengine wapone.

Benchikha ninayemjua mimi ni huyu katika clip hi hapa chini. Ni kocha anayetaka ikibidi kumkunja shati mchezaji wake asiyefuata maelekezo aweze kufanya hivyo. Sasa amekuja kwenye timu anakuta wachezaji wanaitwa magodfather, amekuta macaptain hawaeleweki, wengine ndiyo hao kina Chama wanapelekwa kamati za kina Sirro halafu kesi zao zinaisha juu kwa juu wakati yeye mwenyewe angeweza kulimaliza suala lake. Hapo sijawazungumzia kina Zimbwe, Inonga na Manula. Benchikha aliyeitwa General kabaki kuwa kocha wa kujikunyata kwenye benchi baada ya mechi.

Hana meno. Muondoleeni yoyote yule anayetaka aondoke na mleteeni yoyote yule anayemtaka. Hapo akishindwa ndiyo mumlaumu.




Pitia nyuzi hizi mbili kujua nilichowahi kusema kuhusu Benchikha pale alipokuja tu Simba.

Kwa Benchikha, Simba imeonyesha jeuri ya pesa sasa tunasubiri tuione pia kwa wachezaji wapya

Kosa kubwa limefanyika kumrithisha Benchikha migogoro ya zamani
 
Huyu kocha wana Simba wametokea kumwamini ila kocha hana lolote, Robertinho alikuwa bora zaidi yake. Simba ya Robertinho ilikuwa bora kuliko Simba hii, Benchikha kazidi kuishusha kiwango cha Simba.

Robertinho aikuwa ni mgumu kupoteza mechi dhidi ya timu ndogo kama Mashujaa, Prisons, n.k na ndio maana alikuwa na unbeaten run nzuri sana kabla hajakutana na Yanga.

Ila huyu Benchikha ni tia maji timu ya Simba ina uwiano mmbaya sana wa magoli ya kufungwa na kufunga wakati Robertinho alimaliza ligi na goal difference 58 magoli 15 zaidi ya Yanga waliomaliza kwa 43.
 
Kipimo cha kocha ni kipi?
Timu kucheza vizuri na kupata matokeo.

Sasa mpira mbovu na matokeo hakuna wachezaji haonhaonndo waliowapa makocha wengine waliopita mafanikio. Ugomvi wangu na huyo kocha kwenye kupanga kikosi tu basi
 
Back
Top Bottom