Benin: Mkulima aokotoa furushi lenye mamilioni ya fedha, arudisha kwa mwenyewe

Benin: Mkulima aokotoa furushi lenye mamilioni ya fedha, arudisha kwa mwenyewe

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Mkulima mmoja nchini Benin amepokea tuzo ya heshima kutoka kwa mamlaka ya nchi yake hiyo ni baada ya kuokota mamilioni ya fedha kisha kumrudishia mmiliki.

Fedha hizo aliziokota kwenye begi la kusafiria alilolichukua alipokuwa njiani Ijumaa iliyopita alipokuwa akirejea kutoka shambani kwake.

Baraka Amidou ana umri wa miaka 37, ameoa na baba wa watoto 5 amesema uamuzi wake wa kurejesha fedha hizo, anasema ulichochewa na imani na malezi ya kidini na anasema wala hajutii alichokifanya.

Alitunukiwa cheti cha kutambuliwa na bahasha ya fedha. Kwa mujibu wa mamlaka, ni suala la kumtia moyo na kutambua kitendo chake cha uadilifu.

"Siku hizi tunazidi kushuhudia upotevu wa maadili. Haijapata kutokea kijana ambaye bado ana kila kitu cha kufanya ili kujijenga akafanya kitendo kama hicho,” alisema Djibril Mama Cissé, Gavana wa Borgou, Kaskazini mwa Benin.

Aliokota begi alipokuwa akirudi kutoka shambani kwake. Baada ya kusikia kupitia tangazo la mjini kwamba mwenye nyumba alikuwa akitafuta mfuko huo, alienda kuukabidhi kwa chifu wa kijiji chake.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, begi hilo ni la mfanyabiashara aliyefika kununua nafaka mkoani humo.

Amidou Baraka alikataa CFA 100,000 ambayo mmiliki alitaka kumpa ili kumshukuru. Baada ya kusisitiza, hatimaye alikubali kupokea 50,000 FCFA.


Chanzo: BBC

_123318517_0eaeff0b-38af-40df-bae1-40e653f9a764.jpg


_123318519_b905b941-60bd-4f4a-b82f-e63ad414dc40.jpg
 
Hio pesa kiasi gani ya kupotea pamoja na begi.............hujakabwa...........au ni wallet ilidondoka........acha turudi kwenye bapa la j2
 
Kuna story ya mdanganyika enzi za Mwalimu, za kunyang'anya wahindi na waarabu fedha, wahindi walizificha kwenye madebe wakatupa shambani kwao, huko maporini, mambo yalivyopoa. Kwako uliopita, wakayatafuta wakayapata yote kasoro moja. Wakapotezea, kumbe mfanyakazi wao jamaa akawa analitafuta Kwa Siri, siku 1 akalipata akawarudishia, muhindi akamcheka Sana akamwambia atakufa maskini Hadi Leo huyo Mzee yupo na umaskini wake.
Wahindi walihamia Canada,
Ila anajutiia Sana nafsi Kwa wema ule alioufanya!
 
Africa kila unachosikia tafakari mara kadhaa

Usije ukakuta ni kama issue z yule Billionea alieanza kuokota Mawe ya mabilioni saba sijui sita mara tu baada ya Mzee kusema ameanza kutengeneza Mabilionea Wazalendo…tangu Mzee kaondoka hapati tena yale Mawe ya mabilioni
 
Back
Top Bottom