Habari zenu wakuu
Naam. Ningependa nami kusema machache kutokana na huu uzi. Na pengine kuweka sawa kwa kile ambacho kwa namna mmoja ama nyingine Ni upotoshaji au kutojua ukweli wa Mambo kwa Yale ambayo yametajwa katika Uzi huu uki uliza “BENJAMIN FERNANDES NI NANI!?”
Mleta Uzi angefanya Uzi wake uwe swali na kuorodhesha maswali yake bila Shaka angelipatiwa majibu vizuri tuu, lakini akaamua kujikanyaga kanyaga mwenyewe na kuanza kushusha watu na credibility zao.
Kwa mfano: mwanzoni wa Uzi wake
Selwa anasema
“ .......... Sidhani kabisa kama ni Mtanzania wa kwanza kusoma Harvard maana mtoto wa karamagi anasoma Harvard na kuna watanzania kibao hapo…..”
Halafu cha ajabu kuelekea mwisho wa Uzi wake akacopy na kupaste wasifu wa Benjamin Kutoka Wikipedia
Benjamin Fernandes - Wikipedia . Wasifu ambao una majibu na kuweka sawa hiyo dhana yake
Soma hapa katika nukuu yake.
“....... In 2017, Fernandes became the first Tanzanian in history to attend both Stanford Graduate School of Business and Harvard John F. Kennedy School of Government for an executive education program. ….”
Sasa sijui ndugu yetu huyu kimombo ndio kimemchanganya au hajasoma akaelewa au alicopy na kupaste bila kujua anafanya nini pengine ajaze Uzi wenye na mchanganyiko wa maneno ya kuswahili na kimombo.
Lakini yote sawa, mwandishi anauhuru wa kuandika kwasababu ya ile wanaita freedom of speech lakini akumbuke Uhuru wako uishie pale ambapo wa mwenzako unapoanzia, namaanisha Uhuru wako wa kuongea usiwe sababu ya kupotosha ukweli ama kuchafua watu na heshima zao.
Nami na mjibu Kama ifuatavyo kulingana na kile ulichoandika na Ukiwa bado hujaelewa basi table-teaching pia itahusika
BENJAMIN NA ELIMU YAKE.
Benjamin Fernandes (November 25th, 1992) amepitia hapa Katika safari yake ya elimu.
i. Harvard Kennedy School of Government
2017
Executive Education Program, Rethinking Financial Inclusion.
ii. Stanford University Graduate School of Business.
2015 – 2017
Master of Business Administration (M.B.A.) Administration and Management, General
iii. University of Northwestern - St. Paul. 2010 – 2014
Bachelor's degree, Accounting Major and Minor Computer Science.
iv. Haven of Peace Academy, Dar es Salaam, Tanzania
1998 – 2010.
High school/ secondary and Primary Rejea
https://www.linkedin.com/in/benjaminf7/ utajua kuhusu elimu yake.
Mkuu
Selwa nirudi kwenye Uzi wako pale uliposema.
"... Sidhani kabisa kama ni Mtanzania wa kwanza kusoma Harvard maana mtoto wa karamagi anasoma Harvard na kuna watanzania kibao hapo...Harvard, Princenton na Standford kuna mwaka nilikaribishwa na waTanzanzania wa Princeton nilivoenda kuattend seminar….”
Kutokana na kauli yako hii naomba uungane nami kukujuza kuhusu.
A. Stanford graduate school of business. ambayo Ni moja Kati ya shule Saba tuu zilizopo Stanford University ambazo ni. - The Graduate School of Business
- Graduate School of education
- School of law
- School of medicine
- School of Humanities and sciences
- School of engineering.
- School of Earth, Energy and Environment Sciences.
Fahamu kuwa Kuna watanzania watatu tu Hadi Sasa kusoma hapo Graduate School Of Business ambao Ni.
1. Jonny MBA’2001, ambae anafanya kazi Goldman Sachs, New York
2. Mbwana Alliy MBA’2007, ambae ni mwanzilishi mwenza wa Savannah Fund. Na watatu ni.
3. Benjamin Fernandes MBA'2017 ambae ni mmiliki na mwanzilishi wa NALA, Inc
https://play.google.com/store/apps/details?id=money.nala.pay hao pekee ndio watanzania waliotia mguu hapo school of business. Rejea
https://www.ippmedia.com/en/news/tanzanian-making-history-america-harvard-university (sijui kuhusu hizo schools nyingine 6 zilizobaki Kama wapo sijui Mimi).
Sasa taratibu kabisa nakuomba usome Neno Hadi Neno kwenye nukuuu hii.
“...... He is the first Tanzanian to attend Stanford Graduate School of Business AS AN AFRICA MBA FELLOW and the youngest African to ever be accepted to Stanford Graduate School of Business……”
mkuu nakuomba ukisoma rudia Mara tatu ikiwezekana kutwa Mara tatu iliupone kabisa hiyo dhana yako inayokutafuna. Kwa maelezo kamili Soma makala nzima hapa Wikipedia.
Benjamin Fernandes - Wikipedia
Pia vile vile Rejea maandiko yako uliyocopy na kupaste kwenye Uzi wako bila kuelewa Kutoka Wikipedia.
Bila Shaka hii kadhia ya Stanford University nimeweka sawa na umeelewa ukwanza wa Benjamin pale Stanford tunatakiwa tuusemeje na hivyo ndivyo Benjamin anavyosema Rejea interview
Yake na clouds360.
B. Harvard University. Kumbuka Harvard University Kuna schools 12 ambazo ni
- Harvard Business School
- Harvard School of Dental Medicine
- Harvard Divinity School
- Harvard Law School
- Harvard Kennedy School. Na nyinginezo. Sasa basi
Selwa mnamo. October 8, 2017, Benjamin alianza kupiga kitabu pale Harvard Kennedy School of Government ( wanasemaga Ni shule namba moja kwa maswala ya utawala na serikali/ uongozi duniani) kwa program maalumu ambayo kwa Mara zote huwa inatolea kwa watu wazima (senior 35-50) lakini mtanzania huyu akavunja mwiko huo na kufanya awe
"youngest person in history to be accepted to Harvard Kennedy School of Executive education".
Akiwa na umri wa miaka 24. Elewa hapa tunaongelea Harvard Kennedy School of Government sio Schools nyingine au Harvard University in general Hivyo basi ndio mwezi huo.
“...... October 2017, Fernandes became the FIRST TANZANIAN in history to attend BOTH (Stanford Graduate School of Business - MBA) and (Harvard John F. Kennedy School of Government)........”
ukimaliza kusoma hapa hasa hizo herufi kubwa na Rejea Uzi wako Pia Rejea hapa
Tanzanian making history in America at Harvard University uelewe vizuri sio kuandika andika tuu.
Naona Sasa umeelewa kuhusiana na Harvard, Stanford na Benjamin huku ukiwa unarejea Kama Benjamin anavyosema na ukweli wa Mambo ulivyo