Hapana...yanafanya KAZI mbona...sema machi hizi za caf mfumo wao ni stick...Yani yake mabango hayatembei..yabakuwa yanaonekana Kwa mpangilio ule ..tazama mechi zote hata za sauzi kwenye viwanja wenye LED tv parameters utaona inavyokuwa...
Plus kingine Yale ni mwekezaji kaweka...sio serikali wala tff...wala uwanja wa taifa kina kampuni iliiingia ubia na serikali kufunga zile LED parameters.....so gharama za matangazo kuwa displayed pale ni hao wadhamini wa klabu wanatakiwa kulipa Kwa hiyo kampuni ili matangazo yao yawe displayed...
Kwenye hili nachoona baadhi ya makampuni ni aidha hawako tayari kwenye kulipa au gharama ni kubwa...maana pale unaweza kutwa tangazo linachajiwa Kwa sekunde ..sasa hesabu kampuni idhamini klabu alafu ilipe tena na pesa ya kufanya matangazo yao yaonekane uwanjani.
Hata hivyo ukisema ni wajibu wa klabu kulipia hayo matangazo Kwa kuwa ni wajibu wao kimkataba na hayo makampuni..nayo ni ngumu...maana klabu zinalipa gharama za mchezo .Kisha zilipe tena gharama za ghafla za kudisply matangazo kwenye LED lights za uwanjani..inakuwa ni kichekeshi.
Hivyo basi...huenda klabu zimekataa kulipia hayo matangazo au huenda kampuni zinazodhamini klabu zikawa zimeukataa huo mtego...
Nadhani kuanzia msimu ujao kutakuwa na Sheria ya lazima ya namna ya kutumia hizo LED lights parameters