Benjamin Mkapa Stadium. Je mabango ya matangazo ya umeme yameacha kufanya kazi?

Benjamin Mkapa Stadium. Je mabango ya matangazo ya umeme yameacha kufanya kazi?

Ni takriban miezi miwili tangu kuzinduliwa wa michuano ya African Football League (AFL) ambapo mabango ya matangazo ya umeme yalianza kufanya kazi kwa mara ya kwanza

Lakini katika hali ya kustaajabisha baada ya mechi chache tu kuchezwa uwanjani hapo, mabango hayo hayafanyi kazi tena na badala yake zimebandikwa stickers

Hivi kitu gani hakipo sawa kwetu sisi watanzania?
Ndio maana Azam wao wameamua kutoa tenda kwa mtu kuyasimamia yale mabango
 
Hapana...yanafanya KAZI mbona...sema machi hizi za caf mfumo wao ni stick...Yani yake mabango hayatembei..yabakuwa yanaonekana Kwa mpangilio ule ..tazama mechi zote hata za sauzi kwenye viwanja wenye LED tv parameters utaona inavyokuwa...

Plus kingine Yale ni mwekezaji kaweka...sio serikali wala tff...wala uwanja wa taifa kina kampuni iliiingia ubia na serikali kufunga zile LED parameters.....so gharama za matangazo kuwa displayed pale ni hao wadhamini wa klabu wanatakiwa kulipa Kwa hiyo kampuni ili matangazo yao yawe displayed...

Kwenye hili nachoona baadhi ya makampuni ni aidha hawako tayari kwenye kulipa au gharama ni kubwa...maana pale unaweza kutwa tangazo linachajiwa Kwa sekunde ..sasa hesabu kampuni idhamini klabu alafu ilipe tena na pesa ya kufanya matangazo yao yaonekane uwanjani.

Hata hivyo ukisema ni wajibu wa klabu kulipia hayo matangazo Kwa kuwa ni wajibu wao kimkataba na hayo makampuni..nayo ni ngumu...maana klabu zinalipa gharama za mchezo .Kisha zilipe tena gharama za ghafla za kudisply matangazo kwenye LED lights za uwanjani..inakuwa ni kichekeshi.

Hivyo basi...huenda klabu zimekataa kulipia hayo matangazo au huenda kampuni zinazodhamini klabu zikawa zimeukataa huo mtego...

Nadhani kuanzia msimu ujao kutakuwa na Sheria ya lazima ya namna ya kutumia hizo LED lights parameters

Ndio maana Azam wao wameamua kutoa tenda kwa mtu kuyasimamia yale mabango
Nadhani uko sahihi. Huu utaratibu umekuja katikati ya msimu wakati timu na wadhamini tayari wamepanga bajeti na taratibu zao za msimu mzima. Pia bado uchumi wetu ni mdogo na hakuna mwamko wa kutosha kwenye kutangaza huko maana hata mabango ya Azam naonaga wanatangaza chapati zao tu.
 
Back
Top Bottom