- Source #1
- View Source #1
Wakati mvutano wa vita kati ya Iran, Israel na Marekani ukiendelea Duniani , kumeibuka machapisho yanayosambzwa kwenye mtandao wa Facebook likidai kuwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amejeruhiwa vibaya baada ya shambulizi lililolenga makao ya Mossad jijini Tel Aviv.
- Tunachokijua
- Chanzo kimoja kupitia mtandao wa Facebook kilichapisha taarifa kueleza kuwa waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amejeruhiwa vibaya sana baada ya Iran kushambulia makao makuu ya Mossad, Tel Aviv.
Ufuatiliaji umebaini kuwa Taarifa kuwa Netanyahu amejeruhiwa katika shambulio si ya kweli. Hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo kutoka nchini Israel, ikiwemo ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel.
Aidha Benjamini Netanyahu ameendelea kujirekodi video na kuchapisha katika ukurasa wake wa mtandao wa X (Twitter) akizungumzia vitana inayoendela na haonekani kuwa na majeraha yoyote. Mathalani tizama hapa na hapa.
Kwa kutumia nyenzo za kidijitali za kuchunguza uhalisia wa picha imebainika kuwa picha inayomuonesha Benjamin Netanyahu akiwa hospitalini imetengenezwa kwa teknolojia ya akili unde
Aidha picha hiyo ina kasoro za kimaumbo na haifuati uhalisia wa kibinadamu, hivyo kuthibitisha kuwa si picha halisi.
kando na hilo hakuna uthibitisho kuwa Mossad imeshambuliwa katika makao yake makuu licha mashambulizi kuripotiwa katika baadhi ya maeneo ya Tel Aviv.