Mathias Byabato
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 1,033
- 723
Wanabodi.
Mwandishi Mkongwe wa TBC Benjamini Rwegasira aliyekuwa katika kituo cha Bukoba na baadaye kuungua ugonjwa wa kiharusi kwa kipindi kirefu amefaiki dunia na kuzikwa katika kata ya Gera wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera.
=====
Mazishi ya Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Benjamin Rwegasira aliyefariki dunia Septemba 10, 2024 mkoani Dar es Salaam, yamefanyika leo Septemba 13, 2024 katika makaburi ya familia yaliyopo katika Kijiji cha Kateera Kata ya Gera Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera.
Awali, Ibada ya Misa takatifu ya kumuaga Rwegasira ilifanyika katika makazı ya familia kijijini hapo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt. Ayub Rioba Chacha, Afisa Utumishi Mwandamizi wa shirika hilo Salome Magaya amesema Rwegasira atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa ndani ya TBC.
Akitoa mahubiri Katekista Simon Francis kutoka Parokia ya Mgana Jimbo Katoliki la Bukoba amewataka waumini wa dini ya Kikristo kujiandaa na kifo
===============================
kwa kummbukumbu za waandishi wakongwe unaweza kusoma hapa.
www.jamiiforums.com

Majina ya Watangazaji maarufu enzi hizo Radio Tanzania kabla ya TBC
David Wakati, Sarah Dumba, Eda Sanga, Jacob Tesha, Ananilea Nkya, Sango Kipozi, Omar Jongo, Ahmed Jongo, Barnabas Mluge, Idrissa Sadallah, Benjamin Kikomongo "Ben Kiko", Bartholomeo Kombwa "Bart Kombwa", Danstan Tido Mhando, Masoud Masoud, Yusuph Omar Chunda, Bujaga Izengo Kadago...