chipalila1
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 259
- 32
Ndugu wana jf hivi wafanyakazi wote wa serikar ni lazima mishahara yao ipitie NMB? Kama n kweli kwann hivyo? Wanao jua tafadhar kuhusu hlo watujuze.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sidhani kama wanalazimika kufanya hivyo. Except for waalimu. Taasisi zingine unatumia bank utakayo, ila tu malipo yanachelewa kwa siku kadhaa zaidi kwa ajili ya transactions. Na endapo unapata cheque zozote, inasumbua kama hauna nmb account.
hakuna ulazima wowote wa mtumishi wa serikali kupitishia fedha zake nmb (hususani kupitishia mishahara)
unaweza kutumia benki yeyote ile kutegemea na mazingira uliyopo.
NMB inatumika sana kwa sababu kwanza imesambaa karibu kila wilaya hapa tz sijui kwenye hizi wilaya mpya hivyo basi mtumishi wa serikali anayefanya kazi wilaya ambayo benki pekee iliyopo huko ni nmb kwa utashi mdogo tu lazima atumie nmb kupitishia mshahara wake kuepuka gharama za kuifata benki nyingine makao makuu ya mkoa.
pili serikali inatumia sana benki ya nmb kwa sababu serikali inamiliki shares nyingi sana kweye benki hii kumbukumbu zangu zianaonyesha kwamba serikali ilikuwa inamiliki 51% ya share hadi hivi karibuni ilipoamua kuuza 3% ya share zake kwa watumishi wa benki ya nmb.
Tatu watumishi wengi wa serikali tunatumia benki hii kupitisha mishahara yetu kwa sababu Serikali nayo inaitumia benki hii kuwalipa mishahara watumishi wake, mishahara ya watumishi wa serikali inapelekwa nmb benki ya nmb
ndiyo inasambaza kwenye benki nyingine, hapo sasa ndio kuna ucheleweshaji sisi ambao tunapitishia mshahara wetu nmb tutapata mapema, wale ambao wanapitishia benki nyingine wanachelewa manake hadi nmb waandike cheki nyingine kupeleka kwenye hizo benki kwa hiyo mlolongo unakuwa mrefu, sijui ni ujanja wao ili watumishi tupitishe mishahara yetu nmb. Kwa mf ofisini kwetu watumishi wanaopitishia mishahara yao nmb wanapata mishahara yao mapema kuliko wanaopitishia mishahara yao benki nyingine ambao watasubiri hadi nmb waipeleke kwenye hizo benki nyingine