Benki gani yaweza kunipa huu mtaji?

Benki gani yaweza kunipa huu mtaji?

pale mwanza kuna jengo la gorofa lipo mtaa wa lumumba.
jamaa ni Muha aliingia ubia na mwarabu yeye akatoa kiwanja mwanrabu akatoa pesa za ujenzi wakagawana sehemu za upangishaji baada ya miaka kadhaa mwarabu kupata pesa za upangaji ataondoka na atamwachia jamaa jengo lake.
_kama vipi fanya hivyo kuepukana na stress za bank.
_watakupa miaka 20~30 Ila utakuwa kama mtumwa wao kila mwezi rejesho,na je una garantee gani kuwa miaka hiyo ishirini utakuwa hai na mzima na utakuwa unapata income ya kulipa huo mkopo?
_pia wakati unakopa kuna hela utatakiwa utoe kama valuation,mchanganuo wa mahesabu,garama za mkopo wa bank,rushwa ya maafisa mkopo.....
_kama utaamua kukopa tafakari kwa kina na upate ushauri haswa!

nashukuru sana kwa bank itakua ya mwisho kabisa ka nikishindwa njia Zinngine
 
Nenda Mkombozi Commercial Bank (MCB) wanatoa ushauri mzuri sana na bila shaka wanaweza kukusaidia nariba yao siyo kubwa kulinganishwa na ya mabenki mengine!!!!
 
Kaka nadhani kuna mambo mengi yakuangalia kabla ya kufikia huko unakofikia,

1. Kwa harakaharaka, kwa nyumba kama hiyo unayosema unahitaji si chini ya milion 500 kuisimamisha
2. Kuwa na nyumba ya kuweka Dhamana sio guarantee ya bank kukupa mkopo, cha muhimu wanaangalia utarudishaje huo mkopo, namaanisha hivi una njia gani nyingine (kazi, Biashara) halali ambayo inakupa kipato kitakacholingana na mkopo unaotaka?
3. kwa soko lililopo una uhakika unaweza kulipa deni kwa muda muafaka?

Hata mm nina shida kama yako mkopo wa 500 mln kwa hesabu ya haraka ya calculator utalipa kwa miaka 9 kwa sh 10 mln @ mwezi kama jumla billion 1, je return zako zitamudu hayo marejesho ? km chini ya hapo itakuwa zaidi ya miaka 15

kupata hata mil 800 inawezekana shida ni kwamba kwa hiyo hela unayotaka marejesho utakwama tu ndugu maana kurejesha 10m Kila mwezi itakusumbua sana.mwenzio nina mil 40 NMB narejesha kwa mwaka mmoja..hilo rejesho linanitoa jasho..na biashara ilivyo ngumu..sasa mpaka hiyo nyumba ikamilike marejesho utakua unatoa wap?hebu nenda crdb maana hata mimi nlishaisikia hiyo ya marejesho kwa miaka 30 unaweza kupata maelezo kwa kina..nimekutamani na mpangp wako mzuri..Mungu akufanikishe lengo lako litimie!

Wakuu hamjamjibu kitalaamu inaonekana wote hamjui shida ya mtoa mada mtoa mada haitaji mkopo wa biashara ta kawaida anahitaji mkopo wa biashara wa nyumba kitaalamu tunaita CPF (commercial property Financing) ambavyo vigezo vyake ni tofauti kabisa na majibu yenu.

Kwa kifupi inawezekana yeye kukopeshwa hata kama kipato chake nikidogo na hakiwezi ku meet monthly installment bank inachoangalia ni je ana mikataba inayomwezesha kurudisha lets say 10m TZS @ month? kuna maeneo mengine kabla hujaanza kujenga kuna mabank na makampuni makubwa wana sign mikataba kabisa ya kuonyesha interest au ya kupangisha wanahitaji ramani tu na kurizika na location yenyewe.

Bank inachokifanya ina disburse hela kwa awamu, wanajenga basement lets say na mezzanine halafu watu wanapangisha au wenyewe wanamalzia mpaka juu kwa masharti kuwa all proceeds would be rooted thru the domicile bank na usi diverge to another bank.

Kama sijaeleweka uliza swali nitatoa ufafanuzi zaidi.
 
Mkuu Nguli unafamu benki gani wanaweza kutoa huu mtaji mana umeeleza vema sana hii ishu
 
Back
Top Bottom