Ni access bank pekee, ila uwe mvumilivu mkubwa, kwingine ni mlolongo juu ya mizengwe.
Sijui kwa hapo, ila mwanzoni nilikuwa nayaona majengo yao mpaka pale nilipoona nao wameingia Umoja switch ndio nikapata nafasi ya kuingia ndani nidodose.Na tulioko mikoanai wanakubali au ni lazima niwe mkazi wa Dar?
Bongo hakuna mikopo yenye kuwanufaisha wakopaji ni uwizi na ubabaishaji tu riba wanayocharge na masharti ni very unrealistic and completely unfair.
Hebu fikiria eti kuna wale Blue financial services wana kupa mkopo wa TZS160,000/= na watakiwa kurudha laki 2 in one month?
Wale Easy finance ndio usisema uwizi uwizi mtupu eti wao una mortgage gari, generator au laptop au nyumba ukipeleka gari wao ndio wanaevaluate utaambia gari la 10m thamani yake ni 5m na utapewa mkopo 70% ya mali yako na unakatwa 50,000 ya form, 50,000 ya evaluation na 50,000 loan processing fee na watakiwa kurudisha kwa miezi 3 kwa riba ya 22% WIZI MTUPU..
Sijui Bongo tumelogwa ama vipi hivi hao BOT kazi yao nini?
Kwenye mabenki ndio usiseme mikopo yenyewe masharti kibao mara lete cheti cha babu yako cha kuzaliwa mara riba 22-30% mara pitisha mshahara wako kwenye benki na ukipisha mkopo utausikia hewani au wanakupa mkopo ambao they are sure hutokusaidia chochcote maana riba ni balaaa
Sijajibiwa hapo juu
Mkuu ni kweli kabisa mimi ningeshauri watu wawekeze/save zaidi ya kukopa mabenki au SACCOS ni umaskini
Access Bank ni microfinance Bank wana deal na wateja wadogox2 ambao hawana hata financial informations so interest rates zao ni flat na sio reducing bases hao wanaosema kuna unafuu nawashangaa sana.
Google access bank tz utajionea mwenyewe
wakuu naona tungeomba Jamiiforums ituwekee information kama hizi, ni muhimu sana. Inawezekana wengine tunaendelea kuwa maskini wakati mikopo ya kutuondoka wenye umaskini tunaweza kuipata kiurahisi. Nakubaliana na wanaosema kuwa benki nyingi hapa Tanzania kwenye upande wa mikopo ni wizi mtupu, na ni unyonyaji tu kwa wasio na uwezo na wasio na hope kabisa, hakuna msaada wowote. Lakini kama uwekezaji ndio solution lazima tujue kwamba uwekezaji huwa unaanza na mtaji.........so kama tukiwa na information (which is power) huenda tukaondokana na umaskini haraka.