Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
Mkuu,Mkuu hii mara ya pili naona hoja zako kutokana na huyo Tanzania leaks. Kwa nini unaamini jambo kutoka kwenye page ambayo hata mmilikk pengine humjui
Kuna maelfu ya fake accounts huku mitandoani kuanza humu jf, twitter, insta, Facebook n.k
Mtu anafungua account anaandika anachotaka, tatizo si yeye Bali ni wewe kuamini na kufatilia account ambayo hata mhusika hajulikani.
Mimi hata hizi story za Britannica huwa siziamini wala kuzifuatilia. Hata zile account za machawa zilizopo zenyewe pia siwezi zifatilia sababu ni uongo mtupu, unakuta kaandika Raisi katoa bil 500 wilaya ya tunduru, unakuta hata raisi mwenyewe hajui Kuna hiko kitu
Mimi kanuni yangu katika maisha ni kutoamini, kuhakiki.
Ndiyo maana hata Mungu siamini yupo, kwa sababu sijaweza kuhakiki uwepo wake.
Hiyo habari sikuiamini, lakini pia sikutaka kuipuuza.
Ndiyo maana nikaamua kuihakiki, nikapata ukweli kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya familia.
Nimeona ni habari inayofaa kutukumbusha kuwa tuna wajibu wa kuhakiki hizi habari za wanaharakati online.
Kuna watu wanaamini kila kitu anachoandika Mange Kimambi.
Mange Kimambi kasema FBI wamemkataza asiende kwenye maandamano ubalozi wa Tanzania Marekani.
Watu wanaamini tu.
Nani kahakikisha FBI wamemkataza Mange Kimambi asiende kwenye maandamano hayo?
Tunahitaji kuwahakiki si watawala tu, bali lia hata wanaharakati.
.webp)