joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Vitu vya kujifunza ni vingi sanaTujifunze nini sasa wakati Tanzania inakusanya nusu ya pesa ambazo Kenya inakusanya licha ya kuwa ina ukubwa mara mbili ya Kenya, ina watu milioni 10 zaidi ya Kenya na ina resources nyingi kuliko kenya?
1) Kutumia akili vizuri katika kufikiria mambo kwa ujumla, viongozi wengi na wananchi wengi wa Kenya wanamatatizo makubwa katika hilo. Hivi kama malengo ya biashara yako ni kupata faida ya $400, na ukazipata, na jirani yako malengo yake ni kukusanya $600 akapafanikiwa kupata $500, nani anayefanya vizuri?
2)Ninasisitiza tena, ni muhimu sana Kenya ikajifunza toka kwa Magufuli, huyu jamaa ni mfano wa kuigwa Africa nzima kwa jinsi anavyobadili uchumi wa Tanzania, tabia ya Kenya kutokubaliana na ukweli na kuendelea na sifa za kijinga nchi itasambaratika kama ambavyo Gavana wa Benki kuu ya Kenya anavyosema.
3)Ninakuomba upitie data za mwaka jana za makusanyo ya serikali za Kenya na Tanzania, na ulinganishe na targets za nchi, ndiyo utaachana na mawazo yako ya kizamani, sasa kama Kenya inakusanya zaidi ya Tanzania
i)Kwanini inashindwa kulisha wananchi wake, wakati population yake ni ndogo kuliko ya Tanzania, 10M less?
ii)Kwanini Tanzania imeweza kutoa elimu bure kuanzia Primary schools hadi high school, wakati population yake ni kubwa kuliko Kenya?
iii) Kwanini Tanzania imeweza kuunganisha nchi nzima kwa barabara za lami, Kenya mikoa ya kaskazi mashariki bado hakuna lami wakati Tanzania ni kubwa mara mbili ya Kenya?
iv) Kwanini Unemployment ya Kenya ni mara mbili ya Tanzania wakati population ya Kenya ni ndogo by 10M?