Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 3,118
- 4,238
Ukitaka kukopa ni mserereko tu huendi ofisi yoyote wala humpigii simu yoyote ila ngoma ni wakati wa kulipa hasa unapotaka kufanya mabadiliko ya malipo ya mkopo wako, huwezi ng'o!
Benki hebu acheni hizo bana yaani kuna vitu hivi laiti mngewezesha Watu kujihudumia wenyewe kwenye Mfumo wa ESS (Employee Self Service ESS) basi ingekuwa poa sana.
1. Mtu hawezi kubadili muda na makato ya mkopo bila kufanya top-up. Hii kitu mngeondoa
2. Mtu hawezi kulipa sehemu ya deni analodaiwa na hata akitaka kulipa lote hawezi bila kwenda ofisini, wekeni kila kitu Digitali ili kurahisisha kazi . Kichekesho kingine hiki
3. Mtu hawezi kuuza deni. Mlifanya vema sana kuruhusu mtu kukopa benki yoyote bila kulazimika kupitishwa mshahara wake huko. Hili pia nina imani mnaweza
4. Mtu hawezi kukopa benki nyingine bila kuwa na akaunti kwenye benki hiyo. Kwenye simu tu kuna "tuma kwenda mitandao mingine" nitashangaa kama benki jambo hilo haliwezekani.
Mamlaka zinazohusika zirekebishe mfumo huo na kila kitu kiwe digitali kama ambavyo tunafanya kwenye mchakato wa ukopaji.