Benki ya CRDB itoe ufafanuzi kuhusu akaunti ya diaspora ya tanzanite kama bado ipo au imefungwa

Benki ya CRDB itoe ufafanuzi kuhusu akaunti ya diaspora ya tanzanite kama bado ipo au imefungwa

Richard

Platinum Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
16,890
Reaction score
26,440
Mwaka 2005 benki ya CRDB ilizindua akaunti maalum kwa watanzania ambao walikuwa nje ya mipaka ya Tanzania kwa masomo, biashara ajira au pilikapilika zingine.

Akaunti hiyo ilojulikana kama Tanzanite ailikuwa inamruhusu mteja kuweka kiasi cha fedha humo zikiwemo fedha za kigeni kama dola ya Marekani na pauni Sterling ya Uingereza, ambapo angaweza kuzitumia fedha hizo kama akiba na shughuli zingine pale awapo nchini Tanzania.

Mimi ni mmoja wa watanzania ambao tulishawishiwa na benki hiyo kufungua akaunti hiyo na nakumbuka wakati ule nilipokuwa nchini Uingereza niliwasiliana na mwakilishi wao aliejulikana kwa jina la Chisumo ambae ndiye alieaminiwa na benki hiyo kufanya shughuli zote za kusaidia watanzania kufungua akaunti hiyo.

Taratibu zote zilikamilika na akaunti kuwa hai kiasi cha kuwa na kitabu cha kuwekea fedha yaani pay-in-slip na pia kuwa na Kadi ya Tembo.

Nilijaribu mara mbili tatu hivi, kuweka kiasi cha fedha kama pauni za Uingereza 100 (kwa wakti ule) na nilikuwa nikienda kuweka fedha hizo katika tawi moja la benki ya Lloyds ambalo ndilo lililokuwa likishirikiana na benki ya CRDB katika "scheme" hiyo na tawi hilo lipo katika kitongoji kimoja ambacho kwa sababu mbalimbali sitaweza kulitaja kwa sasa.

Kuna kipindi nilikuwa na shughuli nyingi sana za ujasiriamali na nikasahau hata kuendelea kuweka au kutumia akaunti hiyo na amini usiamini kwa kipindi cha miaka mitani tokea nirudi nyumbani Tanzania nimejaribu mara nyingi kutaka kufahamu kuhusu akaunti hiyo pale CRDB kama ipo bado au imekufa,

Kwa kuwa niliamua kubakia nyumbani Tanzania na kufanya biashara ya kuchoma "chips" na kuku pamoja na vinywaji baridi, nikaona niwe nafuatilia hili suala la hii akaunti ya Tanzanite kutaka kufahamu kama bado ipo na inaendelea kufanya kazi.

Lakini mpaka sasa ufuatiliaji wangu umegonga mwamba na imebidi niweke hili dukuduku langu hapa JF.

Kwa nyakati tofauti nimedokezwa kwamba ile akaunti ilikuwa na mradi wa mtu na hata wengine wakasema kuna mtu ambae alikuwa ana mrija ambao umeelekea kule ofisi ya juu kabisa.

Pia ningependa kufahamu kama ile fedha niliyoweka kama pauni zisizopungua 400 nilizoweka mwaka 2006 bado zitakuwepo katika hiyo akaunti au ndiyo zilikuwa zikikatwa kidogokidogo na sasa hakuna kitu.

Mwisho ningependa kufahamu kwanini CRDB huwa hawapendi kuwasiliana na wateja wao hata kwa njia ya barua pepe ili kuwapa taarifa mbalimbali za kuhusu benki yao na kama kuna mabadiliko yoyote maana walitoa njia zao zote za mawasiliano kama vile namba ya simu ya mkononi na sanduku la posta.

Ningependa kusikia kutoka CRDB kuhusu hii akaunti ya Tanzanite mekaaje imekufa au bado ipo hai na je kama kuna uwezekano wa wateja wa akaunti ya Tanzanite kuweza kufanya maombi upya ili kuboresha taarifa zao ambazo sisi wengine kwa sasa tunaishi Tanzania.

AHSANTE
 
Bank nazo zinakuwa schemes kama product or service!?

Benki nyingi zinafanya hiyo kitu yaitwa Scheme.

Yaani kuna namna fulani watu wanatumia njia ya benki kutengeza pesa kwa aina hiyo.

Lakini zote ni "illegal" na benki ikigundulika yapaswa kulipa faini au pengine mabosi kufikishwa mahakamani.

Fuatilia kesi za aina hiyo kwa Barclays na HSBC ambao ni magwiji wa masuala ya benki duniani.

Kesi ya Libor na Off-shore accounts schemes
 
Duh

Kumbe waliishia kufanya hayo...

Tueleze vizuri kwanini wanakuzungusha, ni acc hawaioni kwenye yao au?
 
Mkuu kama uliweka £400 mwaka 2006 sahau hiyo tena. Na ukifatilia zaidi utaambia unadaiwa.

Ile akaunti ilikuwa ya kwenye mfumo savings account lakini cha kushangaza ilikuwa haitoi riba ila ilikuwa inamakato ya kila mwezi.

Hivyo pesa yako inavyokaa kwao wao walikuwa wanakata percent na badala ya kuongezeka kwa riba kama savings account zingine.

Ile scheme imetafuna pesa za wabeba box wengi sana. Na sababu kubwa ya makato walikuwa wanasema walikuwa wanatunza fedha za kigeni na ukienda watakupa pesa hizo hizo za kigeni badala ya madafu.
 
Mkuu kama uliweka £400 mwaka 2006 sahau hiyo tena. Na ukifatilia zaidi utaambia unadaiwa.

Ile akaunti ilikuwa ya kwenye mfumo savings account lakini cha kushangaza ilikuwa haitoi riba ila ilikuwa inamakato ya kila mwezi.

Hivyo pesa yako inavyokaa kwao wao walikuwa wanakata percent na badala ya kuongezeka kwa riba kama savings account zingine.

Ile scheme imetafuna pesa za wabeba box wengi sana. Na sababu kubwa ya makato walikuwa wanasema walikuwa wanatunza fedha za kigeni na ukienda watakupa pesa hizo hizo za kigeni badala ya madafu.

Nimekupata mkuu.

Lakini ni lazima mtu fulani awajibike kwa hili na uchunguzi ufanyike.
 
Nimekupata mkuu.

Lakini ni lazima mtu fulani awajibike kwa hili na uchunguzi ufanyike.

Mkuu wewe samehe tu na chukulia kama ulitoa sadaka kwenye bonus ya Kimei.
Uchunguzi utafanyika kwenye vingapi ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom