Benki ya CRDB yapunguza viwango vya riba ya mikopo na kuongeza muda wa marejesho kwa watumishi

Kwani ni lazima iwe miaka 7? Itakuaje endapo mtu achague yeye mwenyewe kwa miaka 2?
 
17% bado ni kubwa mnoooo me ngoja niende vikoba tu
 
Kuna jambo huwa silielewi kuhusu hizi taasisi zinazotoa mikopo kwa wafanyakazi! Hivi wafanyakazi wa makampuni binafsi hawaruhusiwi kukopa?maana kila taasisi inatoa mikopo kwa watumishi wa umma/serikali tu!
 
Hongera JPM watakuelewa tu.
Bank zilikuwa zinatumia fedha ya Serikali kuikopesha Serikali
Mkuu! Hivi nikikukopa fedha ili nifungue biashara siku ukija kuhitaji huduma kwenye hiyo biashara yangu(ambayo mtaji nilikopa kwako) napaswa kukuhudumia bure?au ni wewe ndiye unayepaswa kufuata vigezo na masharti ya biashara yangu?
 
Vyuma vimekaa mahala pake tunanyooka tu
 
Hongera JPM watakuelewa tu.
Bank zilikuwa zinatumia fedha ya Serikali kuikopesha Serikali
Naona umekimbilia kutoa hongera wakati muda wa marejesho umeongezwa! Liccm katika ubora wake wa kushangilia kila kitu.


Hongera sana JPM kwa kuleta mvua za kutosha Dar!
 
Hiyo riba ya 17% ni kwa mwaka au nusu mwaka?..... hapo kwenye hizo %ndio watu wanapokuja kujutia...calculation za riba kama unalipa kwa mwaka ni tofauti na miaka 2,3,4...sikwambii hiyo miaka 7.
 
chadema watapinga....na hiii...
 
Kuchukua mkopo wa muda mrefu ni sawa na kujitia kitanzi. Ukitaka kuona manufaa ya mkopo kama kipato ni kikubwa usichukue mkopo unaozidi miaka miwili
 
HAKUNA KILICHOPUNGUZWA HAPO... NI UHUNI TU.. MIAKA IMEONGEZWA 7 TOKA 6.. NA RIBA WAMEPUNGUZA TO 17% KITU NI KILE KILE.. FANYA MATHS UTAONA AT THE END UNALIPA KILE KILE AU ZAIDI. Riba bado kubwa mno mnoooo... mnoooooo... 17% kwa 7 yrs..? Banks zingeweza toa kwa 11% na kupata faida kubwa kwa sbb:

1: watapata wateja wengi sana wakishusha riba to 11%

2: kama BOT wamewashushia banks riba hadi 8% na banks binafsi ikamkopesha mwananchi kwa 11% ana faida ya 3%... Hiyo 3% ni kubwa sana sanaaaa sbb wakishusha to 11% watapata wateja wengi sana na faida yao ya 3% itakuwa kubwaa ..

17% bado kubwa mnoo mnoooooo... Hakuna kitu hapo
 
Mkuu unajua operational cost za hizi benki ?
 
Safiiii JPM.

Vipi wale waliokwisha kopa na hawajamaliza kulipa hili punguzo linawahusu au ndo waendelee kulia ?
 

Je na limit ya kukopa kwa mtumishi wa umma inabakia 50 mil au wameongeza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…