Mm naomba kuuliza kwa wajuzi zaidi,hivi mda ukiongezwa kutoka miaka 6-7 hapo anaefaidika ni mkopoaji au bank?
Natanguliza shukurani
Both lakini zaidi benki. Mteja anafaidika kwa maana ya kulipa kidogo kidogo; badala ya kulipa 800,000 unalipa say, 500,000 (mfano tu lakini). Ila eventually, total amount utakayolipa baada ya muda huo ni kubwa kulika aliyelipa kwa muda mfupi. Huo hapo chini ni MFANO HALISI kutoa BancABC. Kama kipato kinaruhusu, chukua mkopo wa muda mfupi na kama hakiruhusu kwa maana kama utatoka na NIL mwisho mwezi basi huna option zaidi ya kwenda na option ya muda mrefu ila ndio hivyo ujue unapigwa kitu ambacho baadhi hawajui!
====
Kwa miezi 36: 1,282,960.70 x 36 = 46,186,585.20 (benki inachukua 46,186,585.2 - 35,000,000 =
11,186,585.20)
Kwa miezi 24: 1,764,301.60 x 24 = 42,343,238.40 (benki inachukua 42,343,238.40 - 35,000,000 =
7,343,238.40)
Kwa miezi 12: 3,225,480.24 x 12 = 38,705,762.88 (benki inachukua 38,705,762.88 - 35,000,000 =
3,705,762.88)