Benki ya Dunia Kutoa Msaada wa Shilingi Bilioni 700 Kusaidia Kilimo Cha Umwagiliaji Nchini

Benki ya Dunia Kutoa Msaada wa Shilingi Bilioni 700 Kusaidia Kilimo Cha Umwagiliaji Nchini

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Benki ya Dunia WB imeahidi kutoa Msaada wa dola milioni 300 sawa na Bilioni 700 Kwa Ajili ya sekta ya Kilimo.
---
Benki ya Dunia imeahidi kutoa kiasi cha Dola za Marekani milioni 300 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 702 za Tanzania ili kuimarisha miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji nchini Tanzania chini ya mradi wa PforR(Programme for Results Financing).

Ahadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Nathan Balete alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Meneja wa Kilimo kutoka Benki hiyo Holger Kray, ambapo kwa pamoja wamejadiliana kwa kina namna bora ya kukuza na kuimarisha ushirikiano na Benki ya Dunia kwenye sekta Kilimo nchini Tanzania.

Waziri Bashe amesema mchango huo utasaidia kuongeza uhimilivu wa mifumo ya uzalishaji wa chakula
---

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkaazi wa Benki hiyo Kwa Kanda ya Afrika Mashariki Belete Nathan baada kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe..

Pesa hizo zitatolewa chini ya Mpango wa lipa Kwa matokeo na zitalenga zaidi Kilimo Cha Umwagiliaji.

Safi sana naona ajenda ya Kilimo 10/30 "Strong Legacy" ya mapinduzi ya Kilimo inaenda kufikiwa.

Kazi iendelee

=====

FsIfoCGXoAI8DhR
Nimefanya kikao na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Tanzania @WBTanzania Bw. @BeleteNathan akiwa pamoja na Meneja wa Kilimo kutoka Benki hiyo Bw. Holger Kray. Tumejadiliana kwa kina namna bora ya kukuza na kuimarisha ushirikiano na Benki ya Dunia kwenye sekta Kilimo.

Ili kuongeza uhimilivu wa mifumo ya uzalishaji wa chakula; katika kuhakikisha tunaimarisha mifumo ya uzalishaji. @WBTanzania itatoa Dola milioni 300 kwenye kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji nchini chini ya mradi wa PforR(Programme for Results Financing).
 
Ziende kweli kwenye kilimo, maana naanza kupata mashaka hii mikopo ya sasa ni bailout wanatupa nchi ina hali mbaya.
 
Watuwmbie watajenga schemes wapi na zitakuwa za ukubwa gani. Bila hivyo hizi ni pesa za bailout tu.
 
Ziende kweli kwenye kilimo, maana naanza kupata mashaka hii mikopo ya sasa ni bailout wanatupa nchi ina hali mbaya.
Wapi waliposema ni mkopo? Unadhani Nchi 7 zilizochaguliwa kuwa food busket ya Afrika ni Kwa bahati mbaya?

Stay tuned Mkutano mkubwa wa Kilimo unakuja September uta commit matilioni ya shilingi.
 
Wapi waliposema ni mkopo? Unadhani Nchi 7 zilizochaguliwa kuwa food busket ya Afrika ni Kwa bahati mbaya?

Stay tuned Mkutano mkubwa wa Kilimo unakuja September uta commit matilioni ya shilingi.
Unafikiri benki ya dunia ni charity organization?
 
Kipindi tunapokea mikopo tuzingatie na huu ujumbe kama nchi.
 

Attachments

  • 5288027-c00480519c0795dbdaa1810af57dc005.mp4
    9.4 MB
Back
Top Bottom