Benki ya Dunia WB imeahidi kutoa Msaada wa dola milioni 300 sawa na Bilioni 700 Kwa Ajili ya sekta ya Kilimo.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkaazi wa Benki hiyo Kwa Kanda ya Afrika Mashariki Belete Nathan baada kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe..
Pesa hizo zitatolewa chini ya Mpango wa lipa Kwa matokeo na zitalenga zaidi Kilimo Cha Umwagiliaji.
Safi sana naona ajenda ya Kilimo 10/30 "Strong Legacy" ya mapinduzi ya Kilimo inaenda kufikiwa.
Kazi iendelee
=====
Nimefanya kikao na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Tanzania @WBTanzania Bw. @BeleteNathan akiwa pamoja na Meneja wa Kilimo kutoka Benki hiyo Bw. Holger Kray. Tumejadiliana kwa kina namna bora ya kukuza na kuimarisha ushirikiano na Benki ya Dunia kwenye sekta Kilimo.
Ili kuongeza uhimilivu wa mifumo ya uzalishaji wa chakula; katika kuhakikisha tunaimarisha mifumo ya uzalishaji. @WBTanzania itatoa Dola milioni 300 kwenye kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji nchini chini ya mradi wa PforR(Programme for Results Financing).