Benki ya Dunia yachelewesha tena kuipa Tanzania mkopo wa Dola 500M

Benki ya Dunia yachelewesha tena kuipa Tanzania mkopo wa Dola 500M

Hili Tatizo sio dogo wala la kisiasa. Kabla hatujawazuia watoto kusoma shule kwa mimba tuangalieni vyanzo vya mimba utotoni. Tumekuwa na jamii ambayo ni wepisi kulaumu watoto bila kulaumu mila za kizamani na zisizo na maendeleo sehemu nyingine.

Kuna jamii wanaruhusu watoto waolewe wakiwa wadogo sasa serikali hiyo hiyo inasema lazima mtoto asome na serikali hiyo hiyo inasema huwezi kusoma na mimba. Hatutaweza kutatua matatizo kama serikali inafumbua macho mila zetu hasa vijijini. Pili hili Tatizo Vilevile ni la nafasi watoto wa masikini tu ndiyo wataahidwa kusoma.

Ni lazima tuweke sheria ngumu lakini mila zingine nazo tusiziache tu. Hebu tuonyesheni wangapi walio jela kwasababu ya mimba za utotoni!
Hivi mkuu ni kweli kabisa unasema kuwa serikali imefumbia macho suala la mimba za utotoni??? Upo Tanzania hii au??
Hivi hawa watu wanao fungwa kila siku kwasababu ya kuwapa mimba wanafunzi, inamaana huoni mkuu??
Ni mara ngapi wazazi wanakamatwa kwasababu ya kuozesha wanafunzi??
Mkuu nadhani ni sisi hapa JF ndio tumefumba macho kujifanya hatuoni kinachofanywa na serikali.
 
Bank ya Dunia imeona imsikilize Zitto kuliko serikali, ina maana Zitto anaaminika zaidi kuliko serikali yetu tukufu?
Lazima tufikirie kwa nini Benki ya Dunia isikilize hoja za Zitto na sio serikali?

Ina maana wanamwamini sana mwami kuliko kuiamini serikali?
Halafu tuache kumlaumu Zitto tujibu hoja na nchi yetu ni tajiri hao mabeberu wasitutishe hawana lolote na pesa zao wabaki nazo hatuna shida nazo kivile.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Yaani u15 drs la 4 apate mtoto,akishaa zaa arudi darasani kuendelea na wenzake kusoma tena.Kweli tupo serious?Watajifunza nini wenzake?Hatuwaonii huruma wakilimu?

Baadae tukiambiwa system ya elimu yetu ni mbaya tytashangilia kama sasa hivi au?

Tuache ushabiki,masharti ya misaada mingine ni ya kiipuuzi sana.

Watoto si waona kawaida kuwa na watoto wenzao na kuendelea na shule hapo baadae?

Mungu saidia taifa letu!!!
Kama serikali inahitaji sana huu mkopo basi ikubali masharti kuwa watoto wakipata mimba na kuzaa warudi tena kwenye darasa lenye wanafunzi ambao hawajapata mimba na kuzaa kama ambavyo wanaharakati na baadhi ya wanasiasa kama Zitto wanavyotaka!

Yaani, msichana akijisikia kupata mimba anapata na kuzaa halafu baadaye anarudi tena kwenye darasa lake na kuendelea na masomo pamoja na wanafunzi wengine!

Hili suala sio rahisi kama ambavyo baadhi ya washabiki wa wanasiasa wanavyoshangilia ndio maana CHADEMA wameamua kukaa kimya kwa sababu wanajua ugumu wake kijamii na kiimani ya dini!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo sahihi,sio awamu hii ndio imeanza kukataza watoto wakizaa au kuwa na mimba hawana haki ya kurudi shule.Sheria ya katazo Ilikuwepo tangu awamu zilizopita.Tusijifanye hatujui wakati tunajua.

Tukiruhusu heli kama taifa,tutakuwa na taifa la ovyo sana muda si mrefu.

Ya wazungu waachiwe wazungu wenyewe,tusiige kila upuuzi unaopita mbele yetu.
Mkuu jadili ideas sio mipasho

Hapa Tanzania hata kabla ya Rais wa sasa JPM mwanafunzi akipata mimba alikuwa hana haki ya kusoma shule za Kawaida na hata sasa hana haki

Haya mambo ya haki yanahitaji elimu kubwa na ustaarabu wa muda mrefu

Ukiruhusu warudi shule hapa Tanzania hata sisi wengine tutaanza kutembea na wanafunzi kwani bado wa moto

Mataifa ya magharibi wao kila kitu mtu anatakiwa aishi atakavyo lakini usivunje katiba

Ukiwa shoga ni wewe, Ukivuta bangi ni wewe, ukitembea uchi ni wewe

Serikali ikikubali Haya mambo wanafunzi watajazwa sana mimba kwani akipata bado shule atarudi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha magumu kwa familia masikini ni matokeo ya sera mbovu ziletazwo na serikali na hapo hapo inapelekea dhiki inazidi kwenye familia na kufanya watoto wa kike(wanafunzi wa familia za chini) wakose stamina ya kuwakwepa na kushinda vishawishi vya mafataki na hivyo kupelekea mimba shuleni.
WB wanajua kinachoendelea hapa nchini msiwalaumu kwa nini wanamsikiliza sana zito.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom