Benki ya Dunia yachelewesha tena kuipa Tanzania mkopo wa Dola 500M

Hivi mkuu ni kweli kabisa unasema kuwa serikali imefumbia macho suala la mimba za utotoni??? Upo Tanzania hii au??
Hivi hawa watu wanao fungwa kila siku kwasababu ya kuwapa mimba wanafunzi, inamaana huoni mkuu??
Ni mara ngapi wazazi wanakamatwa kwasababu ya kuozesha wanafunzi??
Mkuu nadhani ni sisi hapa JF ndio tumefumba macho kujifanya hatuoni kinachofanywa na serikali.
 
Bank ya Dunia imeona imsikilize Zitto kuliko serikali, ina maana Zitto anaaminika zaidi kuliko serikali yetu tukufu?
Lazima tufikirie kwa nini Benki ya Dunia isikilize hoja za Zitto na sio serikali?

Ina maana wanamwamini sana mwami kuliko kuiamini serikali?
Halafu tuache kumlaumu Zitto tujibu hoja na nchi yetu ni tajiri hao mabeberu wasitutishe hawana lolote na pesa zao wabaki nazo hatuna shida nazo kivile.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Yaani u15 drs la 4 apate mtoto,akishaa zaa arudi darasani kuendelea na wenzake kusoma tena.Kweli tupo serious?Watajifunza nini wenzake?Hatuwaonii huruma wakilimu?

Baadae tukiambiwa system ya elimu yetu ni mbaya tytashangilia kama sasa hivi au?

Tuache ushabiki,masharti ya misaada mingine ni ya kiipuuzi sana.

Watoto si waona kawaida kuwa na watoto wenzao na kuendelea na shule hapo baadae?

Mungu saidia taifa letu!!!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo sahihi,sio awamu hii ndio imeanza kukataza watoto wakizaa au kuwa na mimba hawana haki ya kurudi shule.Sheria ya katazo Ilikuwepo tangu awamu zilizopita.Tusijifanye hatujui wakati tunajua.

Tukiruhusu heli kama taifa,tutakuwa na taifa la ovyo sana muda si mrefu.

Ya wazungu waachiwe wazungu wenyewe,tusiige kila upuuzi unaopita mbele yetu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha magumu kwa familia masikini ni matokeo ya sera mbovu ziletazwo na serikali na hapo hapo inapelekea dhiki inazidi kwenye familia na kufanya watoto wa kike(wanafunzi wa familia za chini) wakose stamina ya kuwakwepa na kushinda vishawishi vya mafataki na hivyo kupelekea mimba shuleni.
WB wanajua kinachoendelea hapa nchini msiwalaumu kwa nini wanamsikiliza sana zito.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…