Benki ya Dunia yaipa Tanzania mkopo wa Tsh Trilioni 1.5

Benki ya Dunia yaipa Tanzania mkopo wa Tsh Trilioni 1.5

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1645514798771.png


Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam

TANZANIA na Benki ya Dunia zimetiliana saini mikataba miwili ya mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya dola za Marekani milioni 650 sawa na shilingi trilioni 1.5 za kitanzania kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya msingi (BOOST) na mradi wa kuimarisha usalama wa umiliki wa ardhi nchini.

Mikataba hiyo imesainiwa Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Tutuba kwa niaba ya Serikali na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Mara Warwick.

Akizungumza baada ya kusainiwa kwa mikataba hiyo, Bw. Tutuba alisema kuwa fedha hizo zimetolewa na Benki ya Dunia kupitia mgao wa masharti nafuu wa Mzunguko wa IDA 19, ambapo dola za Marekani milioni 500 zitatumika kuboresha elimu ya msingi na kiasi kingine cha dola za Marekani milioni 150 kitatumika kuimarisha usalama wa milki za ardhi hapa nchini.

Bw. Tutuba alisema kuwa miradi iliyo chini ya Mikataba iliyosainiwa inatekeleza Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2021/22–2025/26) na ni sehemu ya ajenda kuu ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, inayolenga kujenga uchumi shindani wa viwanda kwa maendeleo ya watu kupitia mikakati mbalimbali.

Alifafanua kuwa katika sekta ya elimu ya msingi, fedha hizo zitatumika kuboresha na kusimamia mazingira shirikishi ya kufundishia na kujifunzia, kuboresha uwezo wa walimu, kukuza na kuhamasisha matumizi ya TEHAMA katika shule za awali na msingi.

Mradi wa BOOST unakusudia kuboresha usawa katika upatikanaji wa elimu bora ya awali na msingi kwa upande wa Tanzania Bara ukiwemo ujenzi wa vyumba 12,000 vya madarasa pamoja na vifaa vinavyohitajika vya elimu; usimikaji wa mifumo na usambazaji wa vifaa vya TEHAMA katika shule na vyuo vya ualimu 800 kwa pamoja; na kuongeza uandikishaji wa wanafunzi kwa shule za awali na msingi.

Bw. Tutuba alisema kuwa katika sekta ya ardhi, kazi zitakazofanyika ni kukuza na kuwezesha upangaji, upimaji na utoaji hatimiliki za ardhi kwa ajili ya uwekezaji na usalama wa makazi ya watu, kuboresha na kuongeza mfumo unganishi wa taarifa za usimamizi wa ardhi na kukuza matumizi ya TEHAMA katika upimaji na uandaaji wa hatimiliki ya ardhi.

“Mradi huu unatarajia kunufaisha nchi kupitia ongezeko la usalama wa umiliki katika wilaya 40 zilizochaguliwa, kwa kutoa hati za Kimila ya Kumiliki Ardhi Vijijini (CCROs), hati za Kumiliki Ardhi Mijini (CROs) na Leseni za Makazi. Aidha, mradi utaongeza ufanisi wa usimamizi wa taarifa za ardhi kupitia uboreshaji wa Mfumo wa Kidijitali wa Taarifa za Ardhi (ILMIS) na utengenezaji wa ramani za msingi (Base Maps)” alifafanua Bw. Tutuba.

“Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, napenda kukushukuru wewe binafsi Bi. Mara Warwick, na kupitia kwako, Benki ya Dunia, kwa mikopo hii muhimu ambayo imekuja katika wakati muafaka” alisema Bw. Tutuba

Aliwaagiza Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi na Katibu MKuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka wakasimamie ukamilishaji kwa masharti yote ya awali (conditions of effectiveness) kwa wakati ili kuwezesha kuanza rasmi kwa utekelezaji wa miradi hiyo miwili.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia hapa nchini Bi. Mara Warwick alisema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuboresha elimu na kwamba fedha zilizotolewa na Benki hiyo kama mkopo nafuu zitawanufaisha zaidi ya wanafunzi 12,000 wanaosoma masomo ya awali na elimu ya msingi.

Bi. Warwick alisema pia kuwa Benki ya Dunia imeidhinisha mkopo wa dola za Marekani milioni 150 kwa sababu mpango wa kuimarisha masuala ya ardhi utawanufaisha zaidi ya wananchi milioni 2 hususan waishio vijiji kwa kupatiwa hatimiliki za kimila zaidi ya 500,000 kwenye mikoa 14 yenye wilaya 40.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka alisema kuwa dola za Marekani milioni 500 sawa na shilingi za Tanzania trilioni 1.15 zitatumika kujenga mazingira mazuri ya kufundisha kwa upande wa walimu na pia kuwawekea wanafunzi miundombinu bora ya kusoma na kuwapatia nyenzo za TEHAMA.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi alisema kuwa kiasi cha dola za Marekani milioni 150 zilizoelekezwa katika kuimarisha sekta ya ardhi, zitatumika kusimika mifumo ya kielektroniki katika mikoa 24 kwa kujenga ofisi za ardhi na kufanya ufuatiliaji na tathimini ya mradi.

Alisema kuwa kiasi cha dola milioni 71.9 kitatumika kuongeza usalama wa ardhi, dola milioni 33.1 (menejimenti ya mifumo) dola milioni 24.7 (Maendeleo ya ardhi), dola milioni 12.7 (Menejimenti ya mradi) na dola za Marekani milioni 7.5 zitaelekezwa kwenye masuala ya dharura na kwamba mradi huo utakapokamilika utaongeza mapato ya Serikali kupitia kodi ya pango la ardhi na mapato mengine ya Serikali.

Kusainiwa kwa mikataba hiyo miwili kumefanya kiwango fedha kilichowekezwa na Benki ya Dunia hapa nchini kufikia dola za Marekani bilioni 6.15 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa hapa nchini katika sekta mbalimbali.

1645467662591_1.jpg

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba (kulia) na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Mara Warwick wakisaini mikataba miwili ya mkopo yenye masharti nafuu ya thamani ya dola za Marekani milioni 650 sawa na shilingi trilioni 1.501 kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya msingi na mradi wa kuimarisha usalama wa milki za ardhi nchini, jijini Dar es Salaam.

1645467661437_2.jpg

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba (kulia) na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Mara Warwick , wakibadilishana hati za mikataba miwili ya mkopo yenye masharti nafuu ya thamani ya dola za Marekani milioni 650 sawa na shilingi trilioni 1.501 kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya msingi na mradi wa kuimarisha usalama wa miliki za ardhi nchini, jijini Dar es Salaam.

1645467659891_3.jpg

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba (kulia) na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Mara Warwick , wakionesha mikataba miwili ya mkopo yenye masharti nafuu ya thamani ya dola za Marekani milioni 650 sawa na shilingi trilioni 1.501 kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya msingi na mradi wa kuimarisha usalama wa miliki za ardhi nchini, jijini Dar es Salaam

1645467660630_4.JPG

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, akizungumza wakati wa halfa ya utiaji saini wa mikataba miwili ya mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya dola za Marekani milioni 650 sawa na shilingi trilioni 1.501 kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya msingi (BOOST) na mradi wa kuimarisha usalama wa milki za ardhi nchini, jijini Dar es Salaam.

1645467656081_5.jpg

Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Mara Warwick, akizungumza wakati wa halfa ya utiaji saini wa mikataba miwili ya mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya dola za Marekani milioni 650 sawa na shilingi trilioni 1.501 kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya msingi na mradi wa kuimarisha usalama wa milki za ardhi nchini, jijini Dar es Salaam.

1645467655822_6.jpg

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi akizungumza wakati wa halfa ya utiaji saini wa mikataba miwili ya mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 650 sawa na shilingi trilioni 1.501 kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya awali na msingi (BOOST) na mradi wa kuimarisha usalama wa milki za ardhi nchini, jijini Dar es Salaam.

1645467657533_7.jpg

Katibu Mkuu wa Wizara ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka, akizungumza wakati wa halfa ya utiaji saini wa mikataba miwili ya mkopo yenye masharti nafuu wenye thamani ya dola za Marekani milioni 650 sawa na shilingi trilioni 1.501 kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya awali na msingi (BOOST) na mradi wa kuimarisha usalama wa milki za ardhi nchini, jijini Dar es Salaam.

1645467649148_8.jpg

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Shaabani( wa kwanza kushoto), Kamishana wa Fedha za Nje wa Wizara hiyo Bi. Sauda Msemo na Kamishna Msaidizi wa Wizara hiyo Bw. Robert Mtengule wakifuatilia hafla ya utiaji saini wa mikataba miwili ya mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya dola za Marekani milioni 650 sawa na shilingi trilioni 1.501 kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya Awali na Msingi (BOOST) na mradi wa kuimarisha usalama wa milki za ardhi nchini, jijini Dar es Salaam.

1645467648396_9.JPG

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba (wa tatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Mara Warwick (wa nne kushoto), pamoja na watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango baada ya kusainiwa mikataba miwili ya mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya dola za Marekani milioni 650 sawa na shilingi trilioni 1.501 kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya Awali na Msingi (BOOST) na mradi wa kuimarisha usalama wa milki za ardhi nchini, jijini Dar es Salaam

1645467647902_10.JPG

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba (wa tatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Mara Warwick( wa nne kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Benki ya Dunia Ofisi ya Dar es Salaam baada ya kusainiwa mikataba miwili ya mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 650 sawa na shilingi trilioni 1.501 kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya Awali na Msingi na mradi wa kuimarisha usalama wa milki za ardhi nchini, jijini Dar es Salaam.
 
This is good news!.
Kazi iendelee.
P

Soma vizuri mkopo kwa ajili ya nini ? “kuimarisha usalama wa umiliki ardhi nchini” hapo kuna uhusiano wa moja kwa moja na uwekezaji na rasilimali zetu.

Huyu raisi wenu siyo kabisa, anyway endeleeni kumuita ” mama” hata kama deep down anawadharau na siajabu hata kuwachukia.
 
Wee Mzee si uliaga rasmi hapa jukwaani? OK uwepo wako ni mzuri kwetu
It's true, niliaga,
nikaenda, nikajaribu, nikaangukia pua, nikarudisha mrejesho

JF ni Naibu, hivyo nimejikuta kwenye uraibu.
P
 
Denia taifa safari hii !!
Mungu ndiye anaejua kitakachotokea .
Tozo ilipoletwa ili ugharamie uendeshaji wa nchi ulitoa macho kama mjusi, ili usiumizwe na makali ya Kodi, basi nchi inabalansi maumivu ya Kodi, maendeleo mengine yanahitajika Sasa, lakini kwa wakati huo hakuna pesa ya kugharamia, mradi wa mwendokasi bila kukopa usingeuona. Msidhani uchumi wetu una nguvu ya kuhimili matumizi, tunaboresha na kuwapa nguvu ya kiuchumi walipa Kodi, wazalishe, deni litajilipa.

Hata Chadema walikuwa wanamkopa Ndesamburo ili kujiendesha
 
It's true, niliaga,
nikaenda, nikajaribu, nikaangukia pua, nikarudisha mrejesho

JF ni Naibu, hivyo nimejikuta kwenye uraibu.
P
Ila umewekeza tayari uchaguzi ujao jina linaweza kurudi, naakutabiria kuchaguliwa kwenye team ya waandishi wa habari wa rais.
Anza kwa kujitolea kwanza, unamwandalia mama documentary nzuri unazipeleka hata TBC Akiziona tu anakufikiria
 
Tozo ilipoletwa ili ugharamie uendeshaji wa nchi ulitoa macho kama mjusi, ili usiumizwe na makali ya Kodi, basi nchi inabalansi maumivu ya Kodi, maendeleo mengine yanahitajika Sasa, lakini kwa wakati huo hakuna pesa ya kugharamia, mradi wa mwendokasi bila kukopa usingeuona. Msidhani uchumi wetu una nguvu ya kuhimili matumizi, tunaboresha na kuwapa nguvu ya kiuchumi walipa Kodi, wazalishe, deni litajilipa.

Hata Chadema walikuwa wanamkopa Ndesamburo ili kujiendesha

Acha ujinga, tozo imewekwa kwa ajili ya kuhudumia na kulipia madeni na siyo kama mnavyodanganywa, au unafikiri haya madeni yanalipwa kwa fedha kutokea wapi ?
 
Soma vizuri mkopo kwa ajili ya nini, “kuimarisha usalama wa umiliki ardhi nchini”
Ningesikia huo mkopo ni kwa ajili ya kwenda kutifua chuma kule mchuchuma na sisi angalau tuingie iron age ingekuwa poa sana; ingekuwa ni mkopo wa kufufua General Tire na maviwanda mengine kama hayo ingekuwa bonge la idea. Dah; hii mikopo ya matundu ya vyoo hatutoboi.
 
Wanakopa kwa hasira kuwakomoa watanganyika..mana kwenye kulipa atakua zake mchambawima akila urojo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hayo masharti ya mkopo ndio yapi?
Tutalipaje huo mkopo?
Tutatumiaje huo mkopo?

Ni vyema kila kitu kikiwekwa wazi kwanza kabla ya kukopa au kukopeshwa.
 
Ningesikia huo mkopo ni kwa ajili ya kwenda kutifua chuma kule mchuchuma na sisi angalau tuingie iron age ingekuwa poa sana; ingekuwa ni mkopo wa kufufua General Tire na maviwanda mengine kama hayo ingekuwa bonge la idea. Dah; hii mikopo ya matundu ya vyoo hatutoboi.

Mkopo uko strategic, Mzungu anataka rasilimali, sheria ya Tanzania ya ardhi hairuhusu mgeni kumiliki ardhi hivyo huo mkopo ni kwa ajili ya kusolve hilo tatizo ili Mzungu achukuwe kila kitu kilichoko chini ya ardhi.
 
Mkopo uko strategic, Mzungu anataka rasilimali, sheria ya Tanzanian ya ardhi hairuhusu mgeni kumiliki ardhi hivyo huo mkopo ni kwa ajili ya solve hilo tatizo ili Mzungu achukuwe kila kitu kilichoko chini ya ardhi.
Dah; tumepigwa manake? Na mkopo tutalipa.
 
Bora hii mikopo ya WORLD BANK na IMF huwa na riba ndogo tofauti na ile ya kibiashara toka mabenki ya kibiashara kama Exim bank,Baclays n.k ambayo marehemu alikuwa akiichukua kwa kufuatwa na kushawishiwa hapa hapa TZ.
 
Back
Top Bottom