Benki ya Dunia yaipa Tanzania mkopo wa Tsh Trilioni 1.5

Benki ya Dunia yaipa Tanzania mkopo wa Tsh Trilioni 1.5

Denia taifa safari hii !!
Mungu ndiye anaejua kitakachotokea .
Acha woga kijana. Kwanza utakuwa umeshakufa. Assumption ni kwamba wote baada ya miaka 100 ijayo hatutakuwepo. Hata anayezaliwa Leo miaka 100 ijayo atakuwa ameshakufa.

Kwa hiyo usiogooe hata ikitokea mtu akajitolea kukupa trilion moja we chukua huwezi jua kesho itakuwaje. Unaweza zichukua halafu mtoa mkopo akafa usiku huohuo ikawa relief kwako.
 
Mama tukumbuke tu watu wako . Loh! Tule wote jamani..
 
It's true, niliaga,
nikaenda, nikajaribu, nikaangukia pua, nikarudisha mrejesho

JF ni Naibu, hivyo nimejikuta kwenye uraibu.
P
Kumbe ulipoaga ulikuwa na malengo fulani?ok pole sana
 
Hivi haya ni nani anaamua au kila mtu anakwenda kujaribu akipewa hewala, Sababu naona watanzania tunapewa tu na kuambiwa mikopo nafuu, mikopo nafuu (unafuu huo sijui upoje) na wala haya mambo huko Mjengoni sisikii kitu.

Au ndio haya Ndugai (Rest in Retirement) alisema
 
Acha ujinga, tozo imewekwa kwa ajili ya kuhudumia na kulipia madeni na siyo kama mnavyodanganywa, au unafikiri haya madeni yanalipwa kwa fedha kutokea wapi ?
Acha undondocha
 
Soma vizuri mkopo kwa ajili ya nini ? “kuimarisha usalama wa umiliki ardhi nchini” hapo kuna uhusiano wa moja kwa moja na uwekezaji na rasilimali zetu.

Huyu raisi wenu siyo kabisa, anyway endeleeni kumuita ” mama” hata kama deep down anawadharau na siajabu hata kuwachukia.
Sababu zinazotolewa za huo mkopo sikuizi hazieleweki, mara mkopo wa miji flani kuwa ya kijani, kuimalisha udalama wa umiliki ardhi ndio nini?? yaani wanaenda kununua vifaa vya kupimia ardhi, kutengeneza hati au nini???
 
Nimeona Tanzania wamepewa mkopo wa trilioni 1.5 kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya miradi mbalimbali

Nimeona ITV taarifa ya habari,mwenye habari kamili aweke
 

Tanzania na Benki ya Dunia zimetiliana saini mikataba miwili ya mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya dola za Marekani milioni 650 sawa na shilingi trilioni 1.5 za kitanzania kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya msingi (BOOST) na mradi wa kuimarisha usalama wa umiliki wa ardhi nchini.
...
Ongeza nyama,kwamba pesa hizo zitatolewa kwa miaka 5 ijayo..

Pili usalama mradi wa kuimarisha usalam wa umiliki ardhi ndio nini?
 
Mkopo uko strategic, Mzungu anataka rasilimali, sheria ya Tanzania ya ardhi hairuhusu mgeni kumiliki ardhi hivyo huo mkopo ni kwa ajili ya kusolve hilo tatizo ili Mzungu achukuwe kila kitu kilichoko chini ya ardhi.
Mkuu Kijakazi you have my respect bila kujali kama uko sahihi au la.
Great Thinker.
 
Ila umewekeza tayari uchaguzi ujao jina linaweza kurudi, naakutabiria kuchaguliwa kwenye team ya waandishi wa habari wa rais.
Anza kwa kujitolea kwanza, unamwandalia mama documentary nzuri unazipeleka hata TBC Akiziona tu anakufikiria
Ndugu yetu mzee Pascal Mayalla yuko almost 60yrs bado unamwombea kazi kwenye timu ya waandishi wa habari wa Rais...!!???

Hata yeye kama bado anatamani mikiki mikiki ya kazi hiyo ktk age hiyo, atakuwa wa ajabu sana...

Mzee Pascal Mayalla achana na wapiga debe hawa. Kaa home tulia na wajukuu, kula pensheni uliyolipwa na kaka yako mwendazake Magufuli...!!
 

Tanzania na Benki ya Dunia zimetiliana saini mikataba miwili ya mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya dola za Marekani milioni 650 sawa na shilingi trilioni 1.5 za kitanzania kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ....
Magufuli alisema hawa huwa wanakopesha kwa vitu vya kijinga sana.
 

Tanzania na Benki ya Dunia zimetiliana saini mikataba miwili ya mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya dola za Marekani milioni 650 sawa na shilingi trilioni...
Sio mcheko...kushoto kulia...mbele nyuma.

Hivi hii mikopo inaenda kule inakostahili kwenda na kufanya yale yaliyokusudiwa? Tanzania itabadilika mno kama kweli tutaitumia ipasavyo hii mikopo
 
Hao usipogusa maslahi yao utakuwa rafiki yao.
Ila ukiwaita mabeberu utaumiap
 
Acha ujinga, tozo imewekwa kwa ajili ya kuhudumia na kulipia madeni na siyo kama mnavyodanganywa, au unafikiri haya madeni yanalipwa kwa fedha kutokea wapi ?
We ulitaka yalipwe kwa fedha kutokea wapi!?
 
Back
Top Bottom