Mkuu
Ally Kombo tafadhali fafanua jinsi bank hiyo itakavyokuwa ina run kupata profit, achana na wanaokejeli kwanza
Je nikikopa nitalipaje
Je nitakatwa bank charges
Je huduma kama fixed account zinakubalika
je vipi huduma kama kuuza na kukua pesa za nje
Nk nk
Hii ni elimu kubwa na watu wanasomea mpaka Shahada ya Umahiri (Masters) na Uzamivu (PhD), mie nakupa "basics" tu za Islamic Banking.
Mwenyezi Mungu SWT anasema kupitia Qur'an, 'ameharamisha riba, na amebariki Biashara' ingawa wako watu wasio na Imani wenye kusema, Biashara ni riba !' na Qur'an (Mwenyezi Mungu) ikaongezea kuwa anaekula riba, basi ametangaza vita na Yeye Mwenyezi Mungu pamoja na Mtume wake. (jiulize: inakuwaje Bank ambayo iko "risk free" na inakula riba lakini bado inafilisika ?)
1. Riba ni nini (Interest)!?
Ni kiasi cha juu kinachoongezwa katika kukopeshwa/mtaji, kinacholipwa kwa muda maalum na mtoaji anahakikisha hayuko katika Hatari yoyote ya kupoteza/ au kupata hasara. Mzigo wote wa gharama na uendeshaji (risk) anabeba mkopaji/mpewa mtaji. Mara nyingi hii inahusiana na Pesa Taslim (Cash).
2. Biashara ni nini ?
Biashara (Trading), ni lazima ihusishe kununua na kuuza bidhaa (buying and selling of goods) and reward or difference is profit (margin), hata Biashara ya kubadilisha pesa ina kuwa na profit inayotokana na tofaouti ya mnunuaji au muuzaji anayokubali kuachia !
Bishara ya Bureau De Change ni halali kabisa, kwani muuza pesa ameweka kiwango cha faida (margin) ambacho ni ile tofauti ambayo unakubali kuiachia wakati wa kununua, au unayolipia wakati wa kuuza (Ksh 1,000/= muuza duka ameinunua kwa Tsh 18,000/= na Mtu/Mteja akihitaji hiyo Ksh 1,000/= anaiuza kwa Tsh 20,000/= tofauti ni Tsh 2,000/= sawa na Ksh 100/= ambayo ndiyo ni Faida) Pesa ikishuka thamani ana pata hasara kama Biashara zingine.
Hivyo Bank yenye mfumo wa uendeshaji wa Kiislaam inaweka misingi na kanuni zake katika Biashara,(kutafuta faida) pia inajihusisha na hasara (profit and loss). Wataalamu wake wanajitahidi kuingia na kufanya Biashara kwa faida, ingawa ikipatikana hasara mnakubaliana jinsi ya kuilipa/fidia !
Zipo aina tofauti (products) za kibenki na kanuni na masharti yake kulingana na aina ya Biashara.
" Mwenyezi Mungu huiondolea baraka "riba" na huzibariki sadaka "QUR'AN: 2:276.