Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) "mgonjwa anayepumulia kwenye mashine"

kasenene

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2008
Posts
1,632
Reaction score
2,413
Mimi kama mdau mkubwa wa Sekta ya kilimo kwa nyakati tofauti tofauti nimetembelea hii benki toka izinduliwe mwaka 2015 na kujaribu kupata mkopo kwa ajili ya shughuli zangu za kilimo na wakati mwingine kujaribu kusaidia wadau wenzangu kupata mikopo lakini katika hali ya kusikitisha saana haya ni baadhi ya mambo ambayo ningependa nikujulishe mwana JF kama unajiandaa kwenda pale jua kuwa utakabiliana nayo;

1. Benki hii mpaka sasa ina matawi manne tu nchi nzima (Dar) tawi moja.

2. Niliponeda 2015 walinambia wao wanatoa mikopo kwa vikundi vidogovidogo tu (i.e AMCOS) pekee.

3. 2017 Nikawapelekea kikundi fulani hapa mkoani kwetu wakasema wao hawana Ofisi Ruvuma hivyo hawatoweza kuwasaidia labda twende NMB. Na pia wanatoa mikopo mikubwa kuanzia 50m ili kuweza kuhimili usimamizi wa mikopo nchini kwani hawana matawi sehemu nyingi na hivyo ni vigumu kusimamia huo mkopo

4. 2019 Nikarudi na kuomba mkopo kwa ajili ya ya kilmo zaidi 500m kupitia kampuni yangu na wadau wangu wachache wakatujibu kwa sasa hawana bodi ya kuweza kuwaruhusu kutoa mikopo mikubwa.

5. Nikajaribu kuomba kuonana na Mkurgenzi wao. Ni bwana mdogo saana alinipa majibu ya chooni ambayo siwezi hata kuyaweka hapa.

Nilipoenda kulalamika wizara ya kilimo wakaniambi ile benki kwa sasa ni kama haina mwelekeo na walifanya makosa wakawabidhi "vijana fulani" na wameharibu hiyo benki hivyo mda si mrefu itavuinjwa kwani imekuwa na makando kando ya kutosha...

Nawasilisha
 
Sasa ile mikopo ya mabilion wanayosema wametoa pesa kwa wakulima maelfu ni data za kupika au.

I think wadau mbalimbali waje watoe ushuhuda jinsi walivyopata mikopo toka TADB
 
Hii bank ilianzishwa kisiasa. Ingefanikiwa ingekua ni jambo la kushangaza sana kwani kifo chake kilionekana lwenye wazo lake tu kabda haijaanzishwa. Wakulima walikua hawajatayarishwa kama ambavyo watendaji wake wenyewe walivyokua hawajatayarishwa na sera zake na product zao hazieleweki
 
Mimi kama mdau mkubwa wa Sekta ya kilimo kwa nyakati tofauti tofauti nimetembelea hii benki toka izinduliwe mwaka 2015 na kujaribu kupata mkopo kwa ajili ya shughuli zangu za kilimo na wakati mwingine kujaribu kusaidia wadau wenzangu kupata mikopo lakini katika hali ya kusikitisha saana haya ni baadhi ya mambo ambayo ningependa nikujulishe mwana JF kama unajiandaa kwenda pale jua kuwa utakabiliana nayo;

1. Benki hii mpaka sasa ina matawi manne tu nchi nzima (Dar) tawi moja.

2. Niliponeda 2015 walinambia wao wanatoa mikopo kwa vikundi vidogovidogo tu (i.e AMCOS) pekee.

3. 2017 Nikawapelekea kikundi fulani hapa mkoani kwetu wakasema wao hawana Ofisi Ruvuma hivyo hawatoweza kuwasaidia labda twende NMB. Na pia wanatoa mikopo mikubwa kuanzia 50m ili kuweza kuhimili usimamizi wa mikopo nchini kwani hawana matawi sehemu nyingi na hivyo ni vigumu kusimamia huo mkopo

4. 2019 Nikarudi na kuomba mkopo kwa ajili ya ya kilmo zaidi 500m kupitia kampuni yangu na wadau wangu wachache wakatujibu kwa sasa hawana bodi ya kuweza kuwaruhusu kutoa mikopo mikubwa.

5. Nikajaribu kuomba kuonana na Mkurgenzi wao. Ni bwana mdogo saana alinipa majibu ya chooni ambayo siwezi hata kuyaweka hapa.

Nilipoenda kulalamika wizara ya kilimo wakaniambi ile benki kwa sasa ni kama haina mwelekeo na walifanya makosa wakawabidhi "vijana fulani" na wameharibu hiyo benki hivyo mda si mrefu itavuinjwa kwani imekuwa na makando kando ya kutosha...

Nawasilisha
Mkuu kasenene akhsante sana kwa huu uzi na pole pia kwa yaliyokupata.
Niliwahi lielezea hili la hii benki humu.
Nami nilienda kutaka mkopo wa 700M, niliyokutana nayo ni hayo umeyaelezea.
Nikaenda PCCB kutoa taarifa,napo nikakutana na upumbavu wa kiwango cha MATAGA.
Tukisema,twaambiwa waongo.
 
Back
Top Bottom