Benki ya NBC yazindua hati fungani ya NBC Twiga Bond riba 10% kwa miaka mitano

Benki ya NBC Yazindua Hati Fungani ya NBC Twiga, kuwainua wajasiriamali na wadau wa kilimo.

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza utoaji wa Dhamana (bondi) ya miaka mitano inayofahamika kama Dhamana ya Twiga NBC, (NBC Twiga Bond) ambayo inamlenga mtu yeyote anayetaka kuwekeza na kupata faida nzuri.

Kiasi cha chini cha ununuzi wa dhamana hiyo ni TZS 500,000 na inaweza kununuliwa kutoka tawi lolote la Benki ya NBC, au Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) wenye leseni ya Dalali.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo jijini DSM leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi alisema, "Kama mmoja wa wakopeshaji wakubwa nchini Tanzania, tunayofuraha kutoa Dhamana yetu (bondi) ya kwanza sokoni iliyopewa jina la Dhamana ya Twiga NBC (NBC Twiga Bond) tukilenga kuongeza TZS300Bn ambazo zitatumika katika kufadhili sekta ndogo na za kati, Kilimo na sekta nyinginezo muhimu kiuchumi nchini.

Mapato yatokanayo na Dhamana ya Twiga yatatuwezesha kukidhi mahitaji ya kifedha kwa ajili ya makundi haya muhimu ambayo yanaajiri watu wengi. Dhamana ya Twiga NBC iko wazi kwa umma, tukimaanisha zinaweza kununuliwa na watu binafsi, makampuni na taasisi. Ni matumaini yetu kuwa hatua hii itakuza ufanisi wa uzalishaji, kuongeza ushindani wa soko, na kutetea kanuni bora za utawala na uwajibikaji katika shughuli za biashara," alisema
Kuna inflation ya 4.5% kwa mwaka, hiyo inamaanisha ni sawa na unapata asilimia 5.5% kwa mwaka, sasa kwa kutumia akili ndogo 2. Kuna Mtanzania atashindwa kuwekeza milioni zake kumi kwenye biashara yoyote alafu ashindwe kutengeneza faida ya milioni ndani ya mwaka?
 
mkuu hii ili ikulipe inakubidii uweke mpunga mrefu milion 60 kwenda juuu

milion 10 ili upate 1 milion kwa mwaka si kweli bora uizungushe mwenyewee
 
Benki ya NBC Yazindua Hati Fungani ya NBC Twiga, kuwainua wajasiriamali na wadau wa kilimo.

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza utoaji wa Dhamana (bondi) ya miaka mitano inayofahamika kama Dhamana ya Twiga NBC, (NBC Twiga Bond) ambayo inamlenga mtu yeyote anayetaka kuwekeza na kupata faida nzuri.

Kiasi cha chini cha ununuzi wa dhamana hiyo ni TZS 500,000 na inaweza kununuliwa kutoka tawi lolote la Benki ya NBC, au Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) wenye leseni ya Dalali.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo jijini DSM leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi alisema, "Kama mmoja wa wakopeshaji wakubwa nchini Tanzania, tunayofuraha kutoa Dhamana yetu (bondi) ya kwanza sokoni iliyopewa jina la Dhamana ya Twiga NBC (NBC Twiga Bond) tukilenga kuongeza TZS300Bn ambazo zitatumika katika kufadhili sekta ndogo na za kati, Kilimo na sekta nyinginezo muhimu kiuchumi nchini.

Mapato yatokanayo na Dhamana ya Twiga yatatuwezesha kukidhi mahitaji ya kifedha kwa ajili ya makundi haya muhimu ambayo yanaajiri watu wengi. Dhamana ya Twiga NBC iko wazi kwa umma, tukimaanisha zinaweza kununuliwa na watu binafsi, makampuni na taasisi. Ni matumaini yetu kuwa hatua hii itakuza ufanisi wa uzalishaji, kuongeza ushindani wa soko, na kutetea kanuni bora za utawala na uwajibikaji katika shughuli za biashara," alisema
Uamuzi ni wako,
Uwekeze hapo NBC kwa mwaka mzima ndio ule hiyo 10% au utafute odds ya 1.13 kwa mhindi ule hiyo hela kwa dakika 90 tu.
 
Watu wanainvest kwenye bond as its less risky,ingekuwa kila mtu anabet anashinda si kila mtu angekuwa tajiri.
 
Hati fungani ni nini?
Kwa uelewa wangu in English ni bond sasa ni kueleze kwa mfano. Serikali inataka kukamilisha project fulani lakini inaamua kwamba mradi huo pesa yake haitotoka serikalini 100% basi inawapa wananchi nafasi ya kushiriki katika utekelezaji wa miradi ndipo hati fungani inatangazwa pamoja na muda na kiasi cha chini cha uwekezaji + faida itakayopatikana katika uwekezaji wako.
Mara nyingi naona wale wenye pesa za kutosha akitia M200 Kwa mwaka 10% kw miaka 5 ni jambo lingine.
 
Nadhani bank zinaanza kucheza mchezo huu.
Hawa ni TCB Tanzania commercial Bank
IMG_20221215_150943.jpg
 
Back
Top Bottom