Nakubaliana nawe mkuu. 16% kwa mwaka ndo almost viwango vinayotumiwa na mabenki kukopesha watu japo vinaenda hadi 24 %. Sasa ukiweka risks na gharama za uendeshaji haiwezekani yakatoa 16 % kwa fixed accounts yatafilisika. Hiyo benki aliyosema ya Exim inatoa 3.5 % tu kwa miezi mitatu kwa kiwango cha pesa kinachozidi milioni 50.
Hii ni investment nzuri na ninaipendekeza kwa wanaoweza kuaffrod kwa sababu ifuatayo>>>
Faida ya mil 38.2 ukitoa asilimia 10 ya tax inabaki 34.38 mil. Kwa wastani ni 2.865 mil. kwa mwaka au 238,750 sh. kwa mwezi.
Which means that mtu mwenye account hiyo ni sawa na mtu mwenye nyumba anayopangisha kwa sh. 238,750 kwa mwezi. Pesa ulizoinvest ni sh mil 61.8 na umeinvest kidogo kidogo. Pesa hiyo usingeweza kupata nyumba ambayo ingekuingizia sh. laki mbili kwa sababu hukuwa nayo at once lakini through this haba na haba umenufaika sawa na mtu aliye na mil. 61.8 cash za kujenga nyumba na kuipangisha. Vilevile kupata kiwanja na kujenga sehemu ambayo utaweza kupangisha kwa sh. laki mbili ni vigumu iwapo capital ni mil. 61 tu.
Kwahiyo, kama mtu ana uwezo wa kuwa na regular income ya kuinvest laki tano kila mwezi namshauri ajiunge na haba na haba account.
Ni kweli exim walikuwa wana-attract deposits kwa riba kubwa ila nafikiri wameshatosheka na viwango huenda vikawa vimeshuka. Ngoja nicheck nao next week then nitaleta update ya viwango hapa kwa faida yetu sote.[Mkuu acha uongo. Exim Bank according to their website kwa kiwango cha zaidi ya mil. 50 wanakupa 3.5 % kwa miezi mitatu na si 16% kama unavyotudanganya hapa ] Niliona tangazo la benki ya exim tawi la temeke pale kwenye ofisi ya TRA na hayo maelezo nilipewa na mfanyakazi wa exim benki sasa sijui mwongo ni mimi au mfanyakazi aliyenipa maelezo
Mkuu asikudanganye mtu hakuna bank inayoweza kukupa asilimia kubwa unless una mipesa mingi mno. nakushauri uwaona taasisi moja inaitwa UNIT TRUST OF TANZANIA inayoendesha mifuko ya UMOJA FUND, WATOTO FUND, JIKIMU FUND na WEKEZA MAISHA FUND. Wako SUKARI HOUSE GHOROFA YA PILI pale karibu na KILIMANJORO HOTEL(HYATT REGENCY HOTEL). Ukiwekeza katika mifuko hii hutarudi tena kuweka hela yako bank, mfano huo mfuko wa UMOJA FUND unatoa si chini ya asilimia 12 kwa mwaka. siwezi kujibu maswali yote lakini nasisitiza nenda pale sukari house 2nd Floor, au tembelea ofisi zao za mikoani ambazo ziko ndani ya ofisi za posta kuu katika mikoa ifuatayo, DODOMA, MBEYA ARUSHA, MWANZA na ZANZIBAR. Hii ni taasisi ambayo iko chini ya wizara ya fedha. nasisitiza hapo ndo mahali pazuri mana hata mimi nina braza yangu yuko ulaya ila nilimshauri awe anatuma hela anawekeza huko, hajajuta mpaka napoandika post hii, sana sana anaona kachelewa.
Mkuu inakuwa ni 16/100*3/12*100,000,000 = 4,000,000 kwa miezi mitatu na si kama ulivyosema kwenye redi.